<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi wa China aagiza kuzuia kutokea mara kwa mara kwa ajali za usalama baada ya ajali mbaya ya moto kwenye duka la mtaani

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 25, 2024

    BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CPC) Jumatano ameagiza kufanya juhudi za kuzuia kutokea mara kwa mara aina mbalimbali za ajali za usalama na kulinda maisha na mali za watu na utulivu wa kijamii, baada ya kutokea kwa ajali mbaya ya moto kwenye duka la mtaani katika mji wa Xinyu, Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China.

    Ajali hiyo ya moto ilitokea majira ya takriban saa 9:30 alasiri kwenye duka la mtaani katika Eneo la Yushui la Mji wa Xinyu. Hadi kufikia sasa, watu 39 wameuawa, wengine tisa kujeruhiwa, na bado kuna watu wanaokwama ndani ya eneo la ajali.

    Rais Xi ameagiza kufanya juhudi kwa nguvu zote kuokoa na kutibu waliojeruhiwa, kuhudumia na kuwajali ipasavyo wafiwa, na kushughulikia athari za ajali hiyo.

    Aidha ametaka kuchunguza chanzo cha moto huo kwa haraka iwezekanavyo, na kuwajibisha waliohusika na ajali hiyo kwa mujibu wa sheria.

    Rais Xi amesisitiza kwamba maeneo mbalimbali ya serikali za mitaa na idara za serikali zinapaswa kujifunza kutokana na ajali hiyo, kuhakikisha utimizaji wajibu wa usalama mahali pa kazi, kuchunguza na kufuatilia kwa makini hatari zinazoweza kutokea, na kutozembea hata kidogo katika kuhakikisha kazi husika inafanywa kwa njia inayofaa.

    Katika maagizo yake, Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, amewataka waokoaji kufanya kazi kwa kunyakua kila dakika katika kutafuta watu ambao bado wanakwama kwenye eneo la ajali, na kufanya bidii kutibu majeruhi na kupunguza athari.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha