<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Barua ya majibu ya Rais wa China yahamasisha wanafunzi wa Kenya wenye moyo wa shukrani

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2024

    Picha hii iliyopigwa Septemba 20, 2023 ikionyesha treni inayoelekea Mombasa ikingoja kwenye Stesheni Kuu ya Nairobi ya reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi iliyojengwa na China jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Han Xu)

    Picha hii iliyopigwa Septemba 20, 2023 ikionyesha treni inayoelekea Mombasa ikingoja kwenye Stesheni Kuu ya Nairobi ya reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi iliyojengwa na China jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Han Xu)

    Jamlick Mwangi Kariuki, Mkenya mwenye umri wa miaka 26 kutoka Mji wa Webuye ulioko Magharibi mwa Kenya, siku zote amekuwa akitafuta njia ya kuonesha shukrani yake kwa fursa kubwa aliyopata kupitia ukaribu wake maalumu kwa China, ambao ulianzia mwaka 2018.

    Kariuki ni mmoja wa kundi la pili la Wakenya 100 waliofadhiliwa kusoma uhandisi nchini China kwa miaka minne, ambao walirudi baada ya kuhitimu na kuchangia ujenzi na utunzaji wa reli ya Kenya.

    “Baada ya kukamilika kwa njia ya reli hiyo (Kenya SGR), ilikuja kufahamika kwamba tulikosa uwezo na utaalam wa kuiendesha na kuitunza. Kwa hivyo ndiyo sababu kulikuwa na programu hii ili kuelimisha wahandisi Wakenya ili waweze kusimamia reli hiyo,” amesema Kariuki, ambaye alirudi Kenya baada ya kupata shahada ya kwanza ya uhandisi katika Chuo Kikuu cha Beijing Jiaotong na kufanya kazi kama mhandisi wa reli kwa Reli ya Mombasa-Nairobi.

    Kwa sasa wafanyakazi wenyeji wanachukua asilimia 80 ya waajiriwa wote wa reli hiyo, wakishikilia vyeo vikiwemo vya kazi za uendeshaji na utunzaji.

    Kariuki aliamua kurudi katika Chuo Kikuu cha Beijing Jiaotong mwaka jana kusomea shahada ya pili ili kutimiza ndoto yake ya kuwa mtaalamu wa reli.

    Wakiwa na hisia za shukrani kwa fursa walizozipata, Kariuki na wanafunzi wenzake pamoja na wahitimu Wakenya wa Chuo Kikuu cha Beijing Jiaotong walimwandikia Rais Xi Jinping barua mwezi wa Oktoba mwaka jana, ili kumshukuru yeye binafsi kwa sababu, Kariuki anasema, “Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kwakweli ni pendekezo lake ili kuhakikisha kwamba tunaunganisha Dunia na kwa ajili ya maendeleo ya wote”.

    Tarehe 17, Januari, Xi aliwajibu barua yao, kwa namna ambayo Kariuki ameielezea kama “barua ndefu sana na ya binafsi”. Xi alisema kwamba amefurahi kuona Wakenya hao wameunganishwa na China kupitia "njia hiyo ya furaha", ambayo ni rejea ya reli ya SGR.

    Kariuki amesema barua yao kwa Xi ilikuwa ya kuonesha shukrani na haikuwa muhimu kukusudia kupata jibu, lakini kwa mshangao wao, Xi aliweza kutenga muda kutoka kwenye ratiba yake yenye shughuli nyingi kuwaandikia barua ya majibu.

    “Kweli inanihamasisha kwamba kiongozi wa China bado ana muda wa kuzingatia jumuiya ya wanafunzi kutoka nchi za nje kwa ujumla wao na kutujali,” amesema.

    Vicky Wangechi Wangari, anayetoka Mji wa Nyahururu ulioko katikati ya Kenya na yuko mwaka wake wa mwisho wa masomo ya shahada ya kwanza, amesema ujumbe alioandika kwenye barua kwa Xi ni “asante elfu kumi”.

    Vicky mwenye umri wa miaka 25 amesema amepata msukumo wa ziada kutoka majibu ya Xi kwa sababu, kama kijana, wakati mwingine anahisi kwamba hakuna mtu anayetambua jitihada zake, ingawa anafanya kazi kwa bidii. “Kisha mtu anaandika jibu na kusema utaendeleza urafiki wa Kenya na China na unaweza kufanikisha.”

    Programu ambayo Kariuki na Vicky wanaishiriki ni mfano wa ushirikiano wa China na Afrika katika kuendeleza vipaji, ambayo imepata nguvu zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

    Kariuki amesema kwamba licha ya barua, walimtumia rais huyu tiketi ya kusafiri kwa reli kutoka Nairobi hadi Mombasa kama zawadi.

    “Rais ametuambia kwamba amepokea tiketi. Ninatumai kwamba ataitumia tiketi hiyo kusafiri kutoka Nairobi hadi Mombasa siku moja. Nadhani itakuwa ni safari nzuri,” amesema.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha