<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping atoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa maofisa wastaafu wa jeshi

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 31, 2024

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa wanajeshi wastaafu wa China aliposhiriki kwenye  sherehe iliyoandaliwa na CMC kwa ajili ya maofisa wastaafu wa kijeshi walioko Beijing, China, Januari 29, 2024. (Xinhua/Li Gang)

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa maofisa wastaafu wa jeshi wa China wakati akishiriki kwenye sherehe iliyoandaliwa na CMC kwa ajili ya maofisa wastaafu wa jeshi walioko Beijing siku ya Jumatatu.

    Majira ya karibu saa kumi jioni, huku kukiwa na makofi ya furaha, Rais Xi alijiunga na maofisa hao wastaafu, akiwauliza juu ya afya na maisha yao. Wamekumbuka kwa pamoja mafanikio makubwa yaliyopatikana na Chama, nchi na jeshi la China katika mwaka uliopita.

    Maofisa hao wastaafu wa jeshi wameeleza kwa kauli moja kushikamana kwa karibu zaidi na Kamati Kuu ya CPC ambayo Komredi Xi Jinping akiwa kiongozi wake mkuu, kufuata kwa uthabiti mwongozo wa Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya, na kutekeleza Fikra ya Xi Jinping juu ya kuimarisha jeshi.

    Wameahidi kutekeleza mfumo wa wajibu wa mwisho kuwa kwa mwenyekiti wa CMC, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kujenga nchi yenye nguvu na kufikia Ustawishaji wa Taifa la China katika sekta zote kwa kupitia maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha