<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi akagua wanajeshi katika Tianjin, na kutoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa wanajeshi wote

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 04, 2024

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu katika   Mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China, Februari 2, 2024. (Xinhua/Li Genge)

    TIANJIN - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) siku ya Ijumaa alikagua vikosi wa wanajeshi katika Tianjin kabla ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ambapo akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama na CMC ametoa salamu za sikukuu kwa askari wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China na Jeshi la Askari Polisi, wafanyakazi wa kiraia wanaofanya kazi katika majeshi, na askari wanamgambo na vikosi vya akiba.

    Siku ya Ijumaa asubuhi, Rais Xi, alikutana na wajumbe wa kamandi ya kijeshi huko Tianjin na kupiga picha pamoja nao.

    Rais Xi amesema kuwa wanajeshi katika Tianjin wametekeleza kwa uthabiti maamuzi na maagizo ya Kamati Kuu ya CPC na CMC katika mwaka uliopita, wamesukuma mbele maendeleo ya kazi mbalimbali kwa hatua madhubuti, na wamekamilisha vizuri majukumu makubwa.

    Rais Xi akipongeza utendaji wa wanajeshi katika kuiunga mkono Tianjin katika juhudi zake za kusaidia kukabiliana na athari za mafuriko, na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya kulinda usalama wa maisha na mali za watu.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, katika mwaka mpya, ni lazima kutekeleza kwa kina mawazo ya Chama juu ya kuimarisha jeshi na mkakati wa kijeshi kwa zama mpya, na kufanya juhudi za kufikia malengo yaliyowekwa kwa ajili ya miaka mia moja ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China ifikapo Mwaka 2027.

    Rais Xi pia amesisitiza kwamba wakati Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2024 unapokaribia, vikosi vya kijeshi vya nchi nzima vinapaswa kuimarisha utayari wa kupambana, kulinda usalama wa nchi na utulivu wa jamii ili kuhakikisha watu wanasherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi zenye shamrashamra, furaha na amani.?

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikutana na wajumbe wa wanajeshi wa China katika Tianjin, Kaskazini mwa China, Februari 2, 2024. (Xinhua/Li Gang)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha