<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi asisitiza kuimarisha uwezo wa raslimali za ardhi ili kuhakikisha maendeleo yenye sifa bora ya mikoa yenye nguvu bora

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 20, 2024

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesisitiza Jumatatu kwamba ni lazima kuimarisha uwezo wa raslimali za ardhi ili kuhakikisha maendeleo yenye sifa bora ya mikoa yenye nguvu bora, na kwamba ni lazima kuongeza uwezo wa usimamizi wa dharura wa mashinani.

    Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametoa maagizo hayo kwenye mkutano wa nne wa kamati ya kuendeleza mageuzi kwa kina na kwa pande zote ya Kamati Kuu ya Chama ambayo yeye ndiye mkurugenzi wake.

    Mkutano huo umepitisha miongozo kuhusu mageuzi ya utaratibu wa usimamizi wa ardhi, kuhimiza kwa pande zote maendeleo ya kijani ya uchumi na jamii ya China, kuongeza uwezo wa usimamizi wa dharura wa mashinani, na kuharakisha uundaji wa utaratibu wa kimsingi wa kuunga mkono uvumbuzi wa pande zote. Pia imepitisha ripoti ya kazi ya kamati hiyo ya Mwaka 2023 pamoja na kazi kuu za kamati hiyo za Mwaka 2024.

    Katika mkutano huo, Rais Xi amesisitiza kuwa utaratibu wa usimamizi wa ardhi unapaswa kuboreshwa ili kuratibu kwa ufanisi zaidi sera za uchumi mkuu na maendeleo ya mikoa ili raslimali za ardhi ziweze kutumika kwa usahihi zaidi na ufanisi wa juu.

    Amesema juhudi zinapaswa kufanywa ili kuongeza uwezo wa raslimali za ardhi katika kuhakikisha maendeleo yenye sifa bora katika mikoa yenye nguvu bora.

    Rais Xi amesema kuhimiza maendeleo ya kijani ya uchumi na jamii ya China ni sera ya kimsingi ya kushughulikia matatizo yanayohusiana na rasilimali, mazingira na ikolojia, na kwamba China itafuata njia ya pande zote, yenye uratibu na uvumbuzi kwa ajili ya kuhimiza maendeleo yasiyoleta uchafuzi kwa mazingira, na kutimiza malengo ya kitaifa ya kufikia kilele cha utoaji wa kaboni kabla ya Mwaka 2030 na kufikia hali ya usawazishaji wa hewa ya kaboni kabla ya Mwaka 2060.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha