<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi asema kujiunga na Rais wa Jamhuri ya Kongo kwa ushirikiano wa kimkakati wenye nguvu zaidi

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 23, 2024

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametumiana salamu za pongezi siku ya Alhamisi na Rais Denis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Kongo kwa kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, na kuahidi kufanya juhudi pamoja na Sassou katika kuendeleza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande hizo mbili akisema.

    Urafiki kati ya China na Jamhuri ya Kongo umeshinda majaribio ya nyakati, Rais Xi amesema.

    Katika miaka 60 iliyopita, ingawa mabadiliko yametokea katika hali ya kimataifa, nchi hizo mbili zimekuwa zikifanya ushirikiano wa dhati na kutafuta maendeleo kwa pamoja, ambapo katika kipindi hicho pande hizo mbili zimekuwa marafiki wazuri na wanaoaminiana kisiasa na washirika wazuri wa ushirikiano wa kiuchumi wenye manufaa kwa pande zote, Rais Xi ameongeza.

    Katika miaka ya hivi karibuni, mawasiliano kati ya nchi hizo mbili yamefanyika mara kwa mara, hali ya kuaminiana kisiasa inaongezeka siku hadi siku, na ushirikiano unaofuata hali halisi yanaendelea kwa hatua madhubuti, yote hayo yameleta matunda dhahiri kwa watu wa nchi hizo mbili, jambo ambalo ni uthibitisho wazi wa moyo wa urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika, Rais Xi amesema.

    Rais wa China amesema anathamini sana maendeleo ya uhusiano wa pande hizo mbili na angependa kufanya juhudi pamoja na Rais Sassou kuchukua maadhimisho hayo ya uhusiano wa nchi mbili kama mwanzo mpya wa kuendeleza zaidi uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Jamhuri ya Congo na kujenga pamoja jumuiya ya kiwango cha juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.

    Kwa upande wake Rais Sassou ameeleza kuwa katika miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia, watu wa nchi zote mbili siku zote wamekuwa na mshikamano na urafiki, wakishikilia matarajio ya pamoja ya amani, haki na ustawi, na kusukuma mbele maendeleo ya haraka ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya Jamhuri ya Kongo na China.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha