Lugha Nyingine
Rais Xi akutana na mwenyekiti wa Bunge la Taifa la Vietnam
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Mwenyekiti wa Bunge la Taifa la Vietnam Vuong Dinh Hue kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Aprili 8, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Mwenyekiti wa Bunge la Taifa la Vietnam Vuong Dinh Hue mjini Beijing siku ya Jumatatu ambapo amemwomba Vuong Dinh Hue afikishe salamu za kirafiki kwa Nguyen Phu Trong, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV), pia amesema katika ziara yake nchini Vietnam mwishoni mwa mwaka jana, yeye na Nguyen Phu Trong walitangaza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja ambayo ina umuhimu wa kimkakati, na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa pande mbili.
Chini ya juhudi za pamoja za pande mbili, makubaliano yaliyofikiwa na yeye na Nguyen Phu Trong yanatekelezwa, Rais Xi ameongeza.
Amesema umaalum wa kipekee wa uhusiano kati ya China na Vietnam ni kwamba pande hizo mbili zina nia sawa na kufuata njia ya maendeleo ya kufanana, na kuwa na mustakabali wa pamoja, na "ukomredi na undugu" ni udhihirisho ulio wazi zaidi wa urafiki wa jadi kati ya vyama hivyo na nchi hizo mbili.
Amesema, pande hizo mbili zinatakiwa kufanya juhudi za pamoja za kuhimiza mafanikio zaidi katika kujenga jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja, kushughulikia vyema ujenzi wa mambo yao ya kisasa, kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya mambo ya ujamaa ya dunia.
Rais Xi amesema, katika wakati wa sasa wa kukabiliwa na mabadiliko na changamano kubwa katika mazingira ya kimataifa na kikanda, maslahi ya pamoja ya China na Vietnam ni kulinda mfumo wa ujamaa na kudumisha utulivu na maendeleo ya kitaifa.
Vuong Dinh Hue amewasilisha salamu za kirafiki na za kutakia kila la kheri kwa Rais Xi kutoka kwa Nguyen Phu Trong, huku akieleza kuwa CPV na serikali ya Vietnam zinapongeza sana maendeleo na hatua kubwa ya China.
Vietnam inafuata kwa uthabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inapinga kwa uthabiti aina yoyote ya shughuli zozote za vikundi vinavyofanya "Taiwan ijitenge", Vuong Dinh Hue amesema.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Mwenyekiti wa Bunge la Taifa la Vietnam Vuong Dinh Hue kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Aprili 8, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
Shughuli ya kuadhimisha Siku ya Mashua ya Qintong 2024 yafanyika Jiangsu, China
Watu watoa heshima kwa marehemu kabla ya siku ya Qingming katika Mji wa Beijing, China
Msanii wa Ethiopia abuni sanaa kutokana na ufunuo wa kitabu maarufu cha China “Yi Jing”
Treni yaendeshwa katikati ya maua karibu na sehemu ya Juyongguan ya Ukuta Mkuu wa Beijing
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma