<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Marais wa China na Ufaransa wahudhuria na kuhutubia ufungaji wa mkutano wa kamati ya wajasiriamali wa China na Ufaransa

    (CRI Online) Mei 07, 2024

    Rais

    (Picha na Zhai Jianlan/Xinhua)

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron alasiri ya jana Mei 6 walihudhuria na kuhutubia ufunguaji wa mkutano wa sita wa kamati ya wajasiriamali wa China na Ufaransa.

    (Picha na Xie Huanchi/Xinhua)

    (Picha na Xie Huanchi/Xinhua)

    Kwenye hotuba yake, Rais Xi amesema huu ni mwaka wa 60 tangu China na Ufaransa zianzishe uhusiano wa kibalozi. Katika miaka 60 iliyopita, nchi hizo mbili zimekuwa wenzi wa ushirikiano wa kunufaishana, na China imekuwa mshirika mkubwa wa kwanza wa kibiashara kwa Ufaransa nje ya Umoja wa Ulaya.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, China ni mwakilishi muhimu wa ustaarabu wa Mashariki, huku Ufaransa ikiwa ni mwakilishi muhimu wa ustaarabu wa Magharibi. Katika hatua mpya ya maendeleo ya binadamu wakati dunia inapokabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayakutokea katika miaka 100 iliyopita, China inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na Ufaransa katika sekta zote, na kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili ufikie kiwango cha juu zaidi na kupata mafanikio makubwa zaidi.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha