Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping awasili Belgrade kwa ziara ya kiserikali nchini Serbia
Usiku wa Mei 7 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China aliwasili Belgrade kwa ndege maalumu kuanza ziara ya kiserikali nchini Serbia kutokana na mwaliko wa Rais Aleksandar Vu?i? wa Jamhuri ya Serbia. (Mpiga picha: Huang Jingwen/XINHUA)
Rais Xi Jinping wa China usiku wa jana Mei 7 aliwasili Belgrade kwa ziara ya kiserikali nchini Serbia.
Kwenye hotuba yake ya maandishi, Rais Xi ameainisha kuwa China na Serbia zina urafiki wa kina, uhusiano wa pande hizo mbili umepitia majaribu kwenye mabadiliko yanayotokea katika mazingira ya kimataifa, na umetoa mfano wa kuigwa kwa mahusiano kati ya nchi mbilimbili. Tangu China na Serbia zilipoanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote mwaka 2016, uhusiano wa nchi hizo mbili umepiga hatua kubwa na kupata mafanikio ya kihistoria.
Rais Xi amesema anatarajia kutumia fursa ya ziara hii, kubadilishana maoni kwa kina na mwenzake wa Serbia Aleksandar Vu?i? kuhusu uhusiano wa pande mbili na masuala mengine wanayoyafuatilia kwa pamoja, na kuweka mpango mpya wa maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili. Rais Xi amesema anaamini kuwa ziara hii hakika itazaa matunda, na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya China na Serbia.
Usiku wa Mei 7 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China aliwasili Belgrade kwa ndege maalumu kuanza ziara ya kiserikali nchini Serbia kutokana na mwaliko wa Rais Aleksandar Vu?i? wa Jamhuri ya Serbia. (Mpiga picha: Liu Bin/XINHUA)
Usiku wa Mei 7 kwa saa za huko, Rais Xi Jinping wa China aliwasili Belgrade kwa ndege maalumu kuanza ziara ya kiserikali nchini Serbia kutokana na mwaliko wa Rais Aleksandar Vu?i? wa Jamhuri ya Serbia. (Mpiga picha: Huang Jingwen/XINHUA)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma