<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi awasili Budapest kwa ziara ya kiserikali nchini Hungary

    (CRI Online) Mei 09, 2024

    Usiku wa tarehe 8, Mei, rais Xi Jinping wa China aliwasili Budapest kwa ndege maalumu,  kuanza ziara yake ya kiserikali nchini Hungary kutokana na mwaliko wa rais wa Hungary Tamas Sulyok na Waziri Mkuu Viktor Orban wa nchi hiyo. Rais Sulyok na mkewe pamoja na viongozi wa serikali ya Hungary waliwakaribisha rais Xi na mkewe kwenye uwanja wa ndege. (Picha na Xie Huanchi/Xinhua)

    Rais Xi Jinping wa China amewasili nchini Hungary kwa ajili ya ziara ya kiserikali nchini humo.

    Katika hotuba ya maandishi aliyoitoa baada ya kuwasili, Rais Xi amesema China na Hungary ni marafiki na washirika wazuri wa kuaminiana, na anafurahi kufanya ziara ya kiserikali nchini Hungary kwa mwaliko wa Rais Tamas Sulyoka na Waziri Mkuu Viktor Orban.

    Amesema Hungary inajulikana kwa historia yake iliyoanzia enzi na dahari na utamaduni wake unaong’aa wa hali mbalibmali, na amewasifi watu wa Hungary wenye bidii na uwerevu.

    Rais Xi pia amesema katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Hungary na watu wake wamekuwa wakipiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ambayo China inayapongeza kwa dhati.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha