<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa Hungary Viktor Orbán wakutana na wanahabari kwa pamoja

    (CRI Online) Mei 10, 2024

    (Picha na Xie Huanchi/Xinhua)

    (Picha na Xie Huanchi/Xinhua)

    Rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa Hungary Viktor Orbán jana Mei 9 walikutana na wanahabari kwa pamoja baada ya kufanya mazungumzo mjini Budapest.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, yeye na Waziri Mkuu Orbán wote wanakubaliana kwamba katika muda mrefu uliopita, China na Hungary siku zote zimekuwa marafiki wakubwa wa kuaminiana na kusaidiana, na pia ni wenzi wema wa ushirikiano wa kunufaishana, kwa hiyo nchi hizo zinastahili kuinua zaidi uhusiano wao na kupanua zaidi wigo wa ushirikiano. Rais Xi amesema anapenda kuchukulia kuanzishwa kwa Uhusiano wa Wenzi wa Kimkakati wa Pande Zote Kwa Hali Zote katika Zama Mpya kati ya China na Hungary kama mwanzo mpya, na kuhimiza uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ufikie ngazi ya juu zaidi.

    Waziri Orbán amesema, China ni nguvu muhimu na chanya kwenye muundo wa dunia yenye ncha nyingi. Hungary inaunga mkono mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na Rais Xi, na kukubali mpango uliotolewa na China kwa ajili ya kutatua migogoro ya kikanda kwa njia ya amani, ikiwemo msukusuko wa Ukraine. Pia amesema, Hungary inatumai kuinua zaidi uhusiano kati yake na China, na kuendelea kuwa wenzi wa ushirikiano kwenye mchakato wa kujijenga kuwa nchi ya kisasa.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha