Lugha Nyingine
Ziara za Rais Xi nchini Ufaransa, Serbia, Hungary zaweka dira kwa siku za baadaye: Waziri wa Mambo ya Nje wa China
BEIJING - Ziara za Rais Xi Jinping wa China nchini Ufaransa, Serbia na Hungary zilizomalizika hivi karibuni zimeimarisha uhusiano kati ya China na nchi hizo tatu za Ulaya na kuupa nguvu mpya ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari, akiirejelea ziara hiyo ya Xi barani Ulaya kama safari ya kusongesha mbele urafiki, kuimarisha hali ya kuaminiana, kuongeza imani na kuweka dira kwa siku za baadaye.
Ameeleza kuwa katika ziara ya Rais Xi nchini Ufaransa, rais wa China amependekeza kulinda uhuru na kujiamuliwa, na kuzuia kwa pamoja vita mpya baridi na mapambano kati ya makundi; kutilia maanani maelewano na kuhimiza kwa pamoja kuishi kwa mapatano katika dunia yenye rangi tofauti; kutupia macho siku za usoni na kushirikiana kuhimiza ujenzi wa dunia yenye ncha nyingi ya usawa na yenye utaratibu; na kushikilia kunufaishana na kupinga kwa pamoja "kutengana kiuchumi."
Pande hizo mbili zimetoa taarifa nne za pamoja kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, akili bandia na usimamizi wa dunia nzima, bioanuwai na bahari, na mawasiliano na ushirikiano wa kilimo, pia zimesaini mikataba karibu 20 ya ushirikiano, Wang amesema.
Katika ziara yake nchini Serbia, Rais Xi na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic wamekubaliana kujenga jumuiya ya China na Serbia yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, na Rais Xi pia ametangaza hatua za awali za China za kuunga mkono ujenzi wa jumuiya hiyo.
Katika ziara yake nchini Hungary, Rais Xi ameonyesha nia ya kuchukua fursa ya kuanzisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote katika hali zote kwa zama mpya kati ya China na Hungary ili kuweka msukumo mpya na wenye nguvu katika ushirikiano kati ya pande hizo mbili, na Hungary inakaribishwa kuwa mwenzi wa China katika njia yake ya kujenga Mambo ya Kisasa ya China.
Kwenye mkutano wa pande tatu huko Paris na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen, Rais Xi amesema hakuna mgogoro wa siasa za kijiografia au mgongano wa kimsingi wa maslahi kati ya China na EU.
Rais Xi amesema uhusiano huo haulengi upande wa tatu, wala hautegemei au kuamrishwa na upande wa tatu, na kwamba China na EU zinapaswa kuendelea kuchukulia kila upande kuwa mwenzi, na kuendelea kushikilia mazungumzo na ushirikiano.
Akijibu kauli ya "uwezo wa uzalishaji kupita mahitaji ya soko la China", Rais Xi ameeleza kuwa kampuni za nishati mpya za China siyo tu zimeboresha usambazaji wa kimataifa na kupunguza shinikizo la mfumuko wa bei duniani, lakini pia zimetoa mchango mkubwa katika mwitikio wa mabadiliko ya tabianchi duniani na uhamaji kuelekea maendeleo ya kijani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma