Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa wito wa juhudi zaidi kuendeleza, kulinda Ukuta Mkuu wa China
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) Jumanne alitoa majibu kwa barua waliyomtumia wanakijiji wa Kijiji cha Shixia cha Eneo la Yanqing la Beijing, na ametoa wito wa kufanya juhudi za kufahamisha watu zaidi kuujua Ukuta Mkuu na kuulinda Ukuta Mkuu ili kurithisha kizazi kwa kizazi mali hiyo yenye thamani ya mababu zetu.
Wakazi wa Kijiji cha Shixia kilichopo karibu na Ukuta Mkuu sehemu ya Badaling hivi majuzi walimwandikia Rais Xi, wakiripoti kazi yao katika kulinda Ukuta Mkuu na mabadiliko yanayotokea katika kijiji hicho.
Katika barua hiyo ya majibu, Rais Xi amesema amefurahishwa kujua kwamba wanakijiji hao wamechukua hatua kwa miaka mingi kulinda Ukuta Mkuu, kurithi utamaduni wa Ukuta Mkuu, na kufuata njia ya ustawishaji kwa kutegemea mali hiyo ya Ukuta Mkuu.
Ukuta Mkuu ni alama wakilishi ya Taifa la China na ishara muhimu ya ustaarabu wa China, Rais Xi amesema. "Ni jukumu letu la pamoja kulinda na kurithisha mabaki ya mali hiyo ya kihistoria na kitamaduni."
Rais Xi ameelezea matumaini yake kwamba wanakijiji hao wataendelea kulinda Ukuta Mkuu kama wanavyolinda maskani yao, kuenzi utamaduni wa Ukuta Mkuu na kusimulia vizuri hadithi kuhusu Ukuta Mkuu.
Ametarajia wanakijiji wengi watashirikishwa na kutoa mchango wao kwa ajili ya kujenga nchi yenye nguvu ya utamaduni ya kijamaa, na kusukuma mbele maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Ukuta Mkuu ni mali kubwa zaidi ya urithi wa kitamaduni nchini China. Tokea Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama, Rais Xi ametilia maanani sana kazi inayohusu kutumia zaidi thamani ya kitamaduni ya Ukuta Mkuu kwa kurithi na kulinda mabaki ya kitamaduni ya Ukuta Mkuu, na kutoa maagizo mara kwa mara juu ya kuhimiza ujenzi wa bustani ya kitaifa ya utamaduni wa Ukuta Mkuu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma