<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Marais Xi na Putin wafanya mazungumzo mjini Beijing, wakiweka dira ya kuimarisha uhusiano

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 17, 2024

    Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Russia Vladimir Putin kwenye uwanja ulio nje ya lango la mashariki la Jumba la Mikutano ya Umma, kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)

    BEIJING – Siku ya Alhamisi mjini Beijing, Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye yuko ziarani nchini China, ambapo pande hizo mbili zimekumbuka kwa pande zote mafanikio yaliyopatikana katika kuendeleza uhusiano kati ya China na Russia, na kubadilishana maoni kwa kina kuhusu uhusiano wa China na Russia na masuala makubwa ya kimataifa na ya kikanda yanayofuatiliwa na pande hizo mbili, wakiweka dira kwa ushirikiano wao katika maeneo mbalimbali.

    Mfano mzuri wa uhusiano wa nchi kubwa

    Rais Xi amesisitiza kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia. Amesema katika robo tatu ya miaka 100 iliyopita, uhusiano kati ya China na Russia umeimarika huku kukikabiliwa na upepo na mvua, na kustahimili majaribu ya mabadiliko ya hali ya kimataifa. Amesema, uhusiano huo umekuwa mfano mzuri kwa nchi kubwa na nchi jirani zao kuheshimiana na kutendeana kwa udhati na unyoofu, na kutafuta urafiki na ushirikiano wa kunufaishana.

    Rais Xi amesema, maendeleo thabiti ya uhusiano kati ya China na Russia si tu kwa maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na watu wa nchi hizo mbili, bali pia yanachangia amani, utulivu na ustawi wa kikanda na dunia kwa ujumla.

    Putin ameeleza furaha yake ya kuzuru China tena baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Russia kwa awamu mpya. Huku akieleza kuwa Rais Xi pia alifanya ziara ya kiserikali nchini Russia mwezi Machi mwaka jana muda mfupi baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais wa China, Putin amesema ni desturi ya kirafiki kati ya nchi hizo mbili, jambo ambalo linadhihirisha kwamba pande zote mbili zinatilia maanani sana kuimarisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Russia katika zama mpya.

    Maendeleo ya uhusiano kati ya Russia na China hayako nje ya manufaa au kulenga upande wowote wa tatu, Rais Putin amesema, huku akiongeza kuwa maendeleo hayo yanasaidia utulivu wa kimkakati wa kimataifa.

    Azma ya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote

    Rais Xi amesema, kutokana na juhudi za pande zote mbili, uhusiano kati ya China na Russia umeendelea kwa hatua madhubuti, uratibu wa kimkakati wa pande zote unaimarishwa, na ushirikiano zaidi katika sekta mbalimbali unaendelea kwa kina, jambo ambalo limetoa mchango chanya katika kudumisha utulivu wa kimkakati wa dunia nzima, na kuhimiza uhusiano wa kimataifa uwe wa kidemokrasia.

    Rais Putin amesema mfumo wa ushirikiano wa kiserikali kati ya Russia na China unaendelea vizuri, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta za uchumi, biashara, kilimo, viwanda, nishati na mafungamano ya mawasiliano umeongezeka kwa kasi.

    Amesema, mwakani, Russia na China zitafanya shughuli za kusherehekea mwaka wa 80 wa ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti.

    Kulinda mfumo wa kimataifa unaotegemea UN

    China na Russia zimejitolea kufanya uratibu wa kimkakati kama msingi wa uhusiano, na kuelekeza usimamizi wa dunia katika mwelekeo sahihi, Rais Xi amesema alipokutana na waandishi wa habari kwa pamoja na Rais Putin.

    “Nchi hizo mbili zimejikita kithabiti katika kulinda mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, na utaratibu wa kimataifa unaotegemea sheria za kimataifa” Rais Xi amesema huku akiongeza kuwa pande hizo zinadumisha uratibu wa karibu na ushirikiano katika majukwaa ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, APEC na G20, na zikiwa zinafuata moyo wa ushirikiano kweli wa pande nyingi, zimehimiza uwepo wa ncha nyingi na utandawazi wa uchumi duniani.

    Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Russia Vladimir Putin kwenye uwanja ulio nje ya lango la mashariki la Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

    Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Russia Vladimir Putin mjini Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)

    Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Russia Vladimir Putin mjini Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)

    Rais Xi Jinping wa China akifanya mkutano wa wahudhuriaji mahsusi na Rais wa Russia Vladimir Putin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Li Tao)

    Rais Xi Jinping wa China akifanya mkutano wa wahudhuriaji mahsusi na Rais wa Russia Vladimir Putin kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Li Tao)

    Rais Xi Jinping wa China na Rais Vladmir Putin wa Russia wakitia saini na kutoa taarifa ya pamoja kuhusu kuzidisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Russia  katika zama mpya kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili baada ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha