<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    China kuzindua shughuli za nchi nzima za kuendeleza urithi wa kitamaduni

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2024

    Watu wakicheza ngoma ya jadi kwenye shughuli za kusherehekea Siku ya Urithi wa Kitamaduni na Kiasili ya China katika Mji wa Kale wa Xiasi wa Kaili, Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Juni 10, 2023. (Picha na Zou Guangxue/Xinhua)

    Watu wakicheza ngoma ya jadi kwenye shughuli za kusherehekea Siku ya Urithi wa Kitamaduni na Kiasili ya China katika Mji wa Kale wa Xiasi wa Kaili, Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Juni 10, 2023. (Picha na Zou Guangxue/Xinhua)

    BEIJING - Shughuli zaidi ya 10,000 za kuendeleza urithi wa kitamaduni usioshikika zitafanyika kote nchini China katika kipindi cha kukaribia Siku ya Urithi wa Kitamaduni na Kiasili ya China, ambayo imepangwa kuadhimishwa Juni 8 mwaka huu, Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China (MCT) imesema siku ya Alhamisi.

    Ikiwa na kaulimbiu ya "kulinda urithi wa kitamaduni, kurithisha ustaarabu," shughuli hiyo ya mwaka huu imechagua Shenyang, mji mkuu wa Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China kuwa mji mwenyeji, Idara ya Kitaifa ya Urithi wa Kitamaduni ya China imesema siku hiyo hiyo.

    Shughuli za kutangaza bidhaa, zikiwemo shughuli 9,642 za nje ya mtandaoni, zikiwemo maonyesho ya kazi za video na picha kuhusu urithi wa kitamaduni usioshikika, pamoja na mihadhara na maonyesho ya sanaa, ofisa wa MCT Hu Yan amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.

    Zaidi ya hayo, serikali za mitaa zitazindua matamasha za ununuzi bidhaa za mambo ya urithi wa kitamaduni usioshikika ili kuendeleza ufufuaji na maendeleo ya manunuzi ya utamaduni na utalii, kwa mujibu wa wizara hiyo.

    Ikiwa ilizinduliwa Mwaka 2006, Siku ya Urithi wa Kitamaduni na Kiasili ya China inafanyika Jumamosi ya pili ya Mwezi Juni kila mwaka. Ilianzishwa kwa nia ya kujenga mazingira mazuri ya kijamii kwa ajili ya kulinda urithi wa kitamaduni na kuendeleza utamaduni mzuri wa jadi wa China. Mji mwenyeji huchaguliwa kila mwaka kufanya shughuli za sherehe.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha