<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Mjumbe maalum wa Rais Xi ashiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Afrika Kusini

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 21, 2024

    JOHANNESBURG - Mjumbe Maalum wa Rais Xi Jinping wa China, Xiao Jie ameshiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa siku ya Jumatano huko Pretoria, mji mkuu wa utawala wa Afrika Kusini.

    Xiao ambaye pia ni naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China ametoa salamu za pongezi na za kutakia kila la kheri za Rais Xi kwa Rais Ramaphosa, akisisitiza kuwa China inatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika Kusini na ingependa kujiunga pamoja na serikali mpya ya Afrika Kusini katika kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua ushirikiano wenye matokeo halisi na kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika Kusini uendelee kwenye ngazi ya juu zaidi.

    Kwa upande wake, Rais Ramaphosa amemshukuru Rais Xi kwa kutuma mjumbe maalum kushiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwake.

    “Serikali mpya ya Afrika Kusini itaendelea kustawisha uhusiano wa kirafiki na China na inatarajia kupanua mawasiliano ya kirafiki na China kwenye ngazi mbalimbali, kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kunufaishana katika sekta mbalimbali, kuimarisha mawasiliano na uratibu katika mambo ya kimataifa, na kusukuma mbele zaidi maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili,” Ramaphosa amesema.?

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha