<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Maonyesho ya mitindo ya Uganda yaonyesha mila, utambulisho wa Kiafrika

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2024

    Mwanamitindo akiwasilisha mavazi yaliyobuniwa kwenye Maonyesho ya Sanaa na Mitindo ya Afrika 2024 (Afri Art and Fashion Show 2024) mjini Kampala, Uganda, Julai 13, 2024. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

    Mwanamitindo akiwasilisha mavazi yaliyobuniwa kwenye Maonyesho ya Sanaa na Mitindo ya Afrika 2024 (Afri Art and Fashion Show 2024) mjini Kampala, Uganda, Julai 13, 2024. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

    KAMPALA - Maonyesho ya Sanaa na Mitindo ya Afrika 2024 (Afri Art and Fashion Show 2024) yenye kaulimbiu ya "Kusherehekea Urembo Wa Kudumu," yamehitimishwa mjini Kampala, Uganda siku ya Jumamosi, huku wasanii na wabunifu zaidi ya 15 wa Afrika wakionyesha kazi za mitindo ya Kiafrika zenye mambo ya kijadi na ya kisasa, zilizowavutia watu.

    Maonyesho hayo ya kila mwaka yameonyesha aina mbalimbali za mavazi na vitu vilivyohamasishwa na mambo ya mila na desturi za Afrika, vilivyoundwa kwa nyenzo za asili kama pamba, nguo za magome ya miti, nyuzi za ndizi, mkonge na kitenge cha kijadi.

    Kwa mujibu wa Cerinah Kasirye, mwanzilishi wa Duka la Trillion Looks ambalo ndiyo waandaji wa maonyesho hayo, jukwaa hilo ni muhimu kwa vijana wenye vipaji kuonesha mitindo yao ya Kiafrika huku ikiendelea kuwa muhimu katika nyakati za kisasa.

    Kasirye amesema kuhifadhi urithi wa Kiafrika ni muhimu katika Dunia ambayo watu wanatafuta utambulisho.

    "Kila mtu anahitaji utambulisho; nimeona waafrika wanaoishi ng’ambo ambao wanatafuta utambulisho. Wanauliza, mimi ni nani?" Kasirye amesema. "Na kwetu sisi, mitindo ni mojawapo ya njia ambazo watu wanaweza kupata utambulisho wao. Watu wanaweza kuhusiana na nguo na vitu tunavyotumia kwa sababu vina urithi mkubwa."

    Amesema vijana wenye vipaji vya mitindo wamekuwa wabunifu zaidi kwa kuingiza mavazi ya kijadi ya Kiafrika kama vile mavazi ya magome ya miti yenye ubunifu wa kisasa. Amesema, nguo ya gome la mti ina historia ya miaka 100, na ni nguo ambayo inapatikana barani Afrika iliyotengenezwa kwa gome la miti.

    Aisha Nabwanika, mmoja wa waonyeshaji katika maonyesho hayo ya mitindo ambaye pia ni mwanzilishi kinara wa utalii wa kitamaduni, amesema Afrika ina urithi mkubwa wa kitamaduni unaoweza kuendelezwa kupitia mitindo.

    Akitoa mfano wa kundi la kabila la Baganda katikati mwa Uganda, ambalo lina kanuni tofauti za mavazi kwa matukio mbalimbali, kama karamu au mazishi, Nabwanika amesema ubunifu huu unafafanua kundi fulani la watu ni nani hasa na ni kitu gani kinawaongoza.

    Mwanamitindo akiwa amesimama kupigwa picha kwenye Maonyesho ya Sanaa na Mitindo ya Afrika 2024 (Afri Art and Fashion Show 2024) mjini Kampala, Uganda, Julai 13, 2024. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

    Mwanamitindo akiwa amesimama kupigwa picha kwenye Maonyesho ya Sanaa na Mitindo ya Afrika 2024 (Afri Art and Fashion Show 2024) mjini Kampala, Uganda, Julai 13, 2024. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha