<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Mtaalamu wa Ethiopia asema ushirikiano kati ya China na Afrika unaendelea licha ya changamoto mbalimbali

    (CRI Online) Septemba 02, 2024

    Mtafiti katika Taasisi ya Elimu ya Sera katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia, Balew Demissie amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika umeshinda majaribu ya muda katika mazingira ya kimataifa yanayobadilika na kuzidi kusonga mbele.

    Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua siku chache kabla ya Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika wiki hii hapa Beijing, Mtafiti huyo amesema urafiki kati ya pande hizo mbili umeshuhudia mabadiliko mengi ya kihistoria pamoja na changamoto mbalimbali.

    Amesema uhusiano kati ya China na Afrika unatokana na urafiki wa pande mbili, uhusiano wa pande nyingi na wa kina, unaojumuisha ushirikiano katika maeneo mengi ikiwemo maendeleo ya uchumi, biashara, utamaduni, elimu, afya, siasa, uongozi, usalama, diplomasia na mawasiliano kati ya watu na watu.

    Bw. Demissie amesema, biashara kati ya pande hizo mbili imekua kwa kiasi kikubwa na kuifanya China kuwa mwenzi mkubwa wa biashara wa Afrika kwa miaka mingi, na kufungua masoko na fursa mpya kwa nchi zinazoibuka barani Afrika.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha