<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping wa China akutana na Rais William Ruto wa Kenya

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 04, 2024

    Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Kenya William Ruto, ambaye yuko Beijing  kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) 2024 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, Septemba 3, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Kenya William Ruto, ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapo ameeleza kuwa nchi hizo mbili zimekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza pamoja ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na kukamilisha miradi mingi ya miundombinu muhimu zaidi, yenye ushawishi zaidi, na ni ya alama zaidi, ikichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya kikanda na kunufaisha watu wa pande hizo mbili.“China na Kenya zinapaswa kufanya juhudi kwa pamoja katika kuendeleza kwa kina na kwa pande zote uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati,” amesema Rais Xi.

    Amependekeza nchi hizo mbili kuendelea kudumisha urafiki wao na kuendelea kuwa washirika wa dhati wanaoaminiana.

    Pande hizo mbili zinapaswa kuoanisha ujenzi wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na mpango wa uchumi wa Kenya wa “Matarajio ya 2030”, na kuimarisha ushirikiano katika uchumi wa kidijitali, nishati mpya, uchumi, biashara, kupunguza umaskini na maeneo mengine, Rais Xi amesema.

    Amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa mawasiliano na uratibu kati ya nchi hizo mbili katika masuala ya kimataifa na kikanda ili kulinda kwa pamoja maslahi ya pamoja ya nchi za Kusini na kuhimiza amani na utulivu wa kikanda.

    Kwa upande wake Rais Ruto ameelezea matumaini kuwa mkutano wa kilele wa FOCAC utasaidia kuendeleza zaidi uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya Kenya na China.

    Amesema Kenya inakaribisha upande wa China kuendelea kujitahidi kuongeza uwekezaji nchini Kenya na kupanua ushirikiano wenye matokeo halisi katika sekta mbalimbali, hususan katika mafungamano ya mawasiliano, nishati mpya na maendeleo ya vijana.

    Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Kenya William Ruto, ambaye yuko Beijing  kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) 2024 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, Septemba 3, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha