<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais wa DRC asema China ni mwenzi wa kutegemeka wa Afrika

    (CRI Online) Septemba 05, 2024

    Felix Tshisekedi

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi (mbele katikati)

    ?(Xinhua/Shi Yu)

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi amesema China imedhihirishwa kuwa ni mwenzi wa kutegemeka katika maendeleo ya bara la Afrika.

    Akizungumza siku chache kabla ya kuhudhuria mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaofanyika hapa Beijing, Rais Tshisekedi amesema, chini ya mifumo kama FOCAC, miradi mingi ya ushirikiano imetekelezwa nchini DRC, na kutolea mfano mradi wa bandari kavu ya Sakania, kituo cha kuzalisha umeme cha Busanga, na kituo kidogo cha Kinsuka.

    Wakati huohuo, rais Tshisekedi amepinga madai kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika ni ‘mtego wa madeni,’ akisema madai hayo hayaendani na ukweli wa ushirikiano kati ya China na Afrika ambao umeonekana nchini DRC. Ameongeza kuwa, uwekezaji unaofanywa na China umeiwezesha DRC kuendeleza miundombinu yake muhimu na kuimarisha uwezo wake wa kuingia katika uchumi wa dunia.

    Rais Tshisekedi amesisitiza umuhimu wa FOCAC katika kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakbali wa pamoja, akisema ushirikiano kati ya pande hizo mbili ni muhimu katika kuibuka kwa nchi za Kusini.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha