<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Katibu Mkuu wa UN asema ushirikiano kati ya China na Afrika ni nguzo kuu ya ushirikiano kati ya Kusini na Kusini

    (CRI Online) Septemba 06, 2024

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika ni nguzo kuu ya ushirikiano wa kimataifa kati ya Kusini na Kusini, na juhudi za pamoja kati ya China na Afrika zitatoa msukumo mpya kwa maendeleo ya Bara la Afrika.

    Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika jana Alhamisi hapa Beijing, Bw. Guterres amesema China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika, na amepongeza hatua 10 zilizotangazwa na rais wa China Xi Jinping kuhusu ushirikiano wa China na Afrika kwenye kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa.

    Bw. Guterres amesema mafanikio makubwa ya China katika kutokomeza umaskini na masuala mengine yatatoa uzoefu na ujuzi mwingi kwa maendeleo ya Afrika.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha