<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Mazungumzo ya Kwanza ya Mawaziri wa China na nchi za Afrika Mashariki kuhusu Ushirikiano wa Utekelezaji wa Sheria na Usalama wafanyika Beijing

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 09, 2024

    Mjumbe wa taifa na Waziri wa Usalama wa Umma wa China Wang Xiaohong na Waziri wa Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma wa Burundi Martin Niteretse wakishiriki kwenye mazungumzo ya kwanza ya Mawaziri wa China na Afrika Mashariki kuhusu Ushirikiano wa Utekelezaji wa Sheria na Usalama na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, China, Septemba 7, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

    Mjumbe wa taifa na Waziri wa Usalama wa Umma wa China Wang Xiaohong na Waziri wa Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma wa Burundi Martin Niteretse wakishiriki kwenye mazungumzo ya kwanza ya Mawaziri wa China na nchi za Afrika Mashariki kuhusu Ushirikiano wa Utekelezaji wa Sheria na Usalama na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, China, Septemba 7, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

    BEIJING - Mazungumzo ya kwanza ya Mawaziri wa China na nchi za Afrika Mashariki kuhusu Ushirikiano wa Utekelezaji wa Sheria na Usalama yamefanyika Beijing siku ya Jumamosi ambapo mazungumzo hayo yamelenga kutoa dhamana ya hali ya juu ya usalama na ustawi wa pamoja kati ya China na nchi za Afrika Mashariki.

    Mjumbe wa Taifa na Waziri wa Usalama wa Umma wa China Wang Xiaohong na Waziri wa Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma wa Burundi Martin Niteretse waliongoza mazungumzo hayo.

    Wang amebainisha kuwa uhusiano wa pande mbili kati ya China na nchi zote za Afrika ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na China umepandishwa kuwa wa uhusiano wa kimkakati, na kwamba hali ya jumla ya sifa ya uhusiano kati ya China na Afrika imeinuliwa na kuwa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote za hewa kwa zama mpya.

    Wang amesema China ina nia ya kushirikiana na nchi za Afrika Mashariki kuhimiza utekelezaji wa Pendekezo la Usalama wa Dunia, kujenga jukwaa jipya la mazungumzo ya pande nyingi, kushughulikia changamoto mpya katika utekelezaji wa sheria na usalama, kuhimiza hatua mpya kwa ajili ya kujenga uwezo, na kuunda mwenendo mpya wa ushirikiano wa utekelezaji wa sheria na usalama kati ya China na Afrika Mashariki katika zama mpya.

    Mjumbe wa taifa na Waziri wa Usalama wa Umma wa China Wang Xiaohong na Waziri wa Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma wa Burundi Martin Niteretse wakishiriki kwenye mazungumzo ya kwanza ya Mawaziri wa China na Afrika Mashariki kuhusu Ushirikiano wa Utekelezaji wa Sheria na Usalama na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, China, Septemba 7, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

    Mjumbe wa taifa na Waziri wa Usalama wa Umma wa China Wang Xiaohong na Waziri wa Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii na Usalama wa Umma wa Burundi Martin Niteretse wakishiriki kwenye mazungumzo ya kwanza ya Mawaziri wa China na Afrika Mashariki kuhusu Ushirikiano wa Utekelezaji wa Sheria na Usalama na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, China, Septemba 7, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

    Siku hiyo hiyo, Wang alikutana na Niteretse na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jacquemain Shabani.

    Akizungumza na Shabani, Wang amesema kuwa China itashirikiana na DRC kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuimarisha mawasiliano ya wataalam, na kuzidisha ushirikiano wenye matokeo halisi katika maeneo kama vile usalama na kujenga uwezo wa utekelezaji sheria chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

    Kwa upande wake, Shabani ametoa shukrani kwa uungaji mkono muhimu wa China, akisema kuwa DRC inafuata kwa dhati kanuni ya kuwepo kwa China moja na itachukua hatua madhubuti kuimarisha usalama wa kampuni na wafanyakazi wa China nchini humo.

    Mjumbe wa Taifa na Waziri wa Usalama wa Umma wa China Wang Xiaohong akikutana na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kidermokrasia ya Kongo (DRC), Jacquemain Shabani mjini Beijing, China, Septemba 7, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

    Kwenye mkutano wake na Niteretse, Wang amesema kuwa China itazidisha ushirikiano wenye matokeo halisi katika utekelezaji wa sheria na usalama, na kuhimiza maendeleo ya ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Burundi kwa ngazi ya juu na wigo mpana zaidi.

    Kwa upande wake Niteretse amesema, Burundi ina nia ya kuiunga mkono China kwa uthabiti katika masuala yanayohusiana na maslahi makuu ya China, kufanya kazi pamoja ipasavyo ili kutekeleza kwa ufanisi matokeo ya mazungumzo hayo ya mawaziri, na kuhimiza maendeleo ya ngazi ya juu ya ushirikiano katika utekelezaji wa sheria na usalama.?

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha