<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Kituo kipya cha usambazaji cha Shandong?cha reli ya China-Ulaya chazinduliwa nchini Serbia

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 09, 2024

    Treni ya kwanza ya mnyororo maalum wa usambazaji ya kampuni ya Matairi ya Shandong Linglong ya Reli ya China-Ulaya ikiwasili Indjija, Belgrade, Septemba 7, 2024. (Picha na Wang Wei/Xinhua)

    Treni ya kwanza ya mnyororo maalum wa usambazaji ya kampuni ya Matairi ya Shandong Linglong ya Reli ya China-Ulaya ikiwasili Indjija, Belgrade, Septemba 7, 2024. (Picha na Wang Wei/Xinhua)

    INDJIJA, Serbia - Kituo cha usambazaji cha Shandong cha Reli ya China-Ulaya kimezinduliwa mwishoni mwa wiki siku ya Jumamosi kwenye hafla iliyofanyika Indjija, mji ulioko umbali wa kilomita 50 kaskazini magharibi mwa Belgrade.

    Hafla hiyo, ambayo pia ilishuhudia kukamilika na kukabidhiwa kwa treni ya kwanza ya maalumu ya myororo wa usambazaji ya kampuni ya matairi ya Shandong Linglong, ilihudhuriwa na maafisa wa serikali na wawakilishi wa sekta hiyo kutoka Serbia na China.

    Tomislav Momirovic, waziri wa biashara ya ndani na nje wa Serbia, amesema kituo hicho kitatoa mchango muhimu katika kuendeleza miundombinu na miradi ya nishati ya Serbia, kikiiweka nchi hiyo kuwa muhimu cha usambazaji katika kanda.

    Zhang Zhe, kaimu balozi wa Ubalozi wa China nchini Serbia, amehimiza wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili kuboresha ushirikiano kati yao na kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha