<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    China yaunga mkono utoaji wa msaada?endelevu wa kifedha kwa operesheni za kulinda amani zinazoongozwa na AU

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 10, 2024

    UMOJA WA MATAIFA - China inaunga mkono utoaji wa msaada endelevu wa kifedha ambao ni wa kutosha, unaokadiriwa na endelevu kwa ajili ya operesheni za amani za Afrika zinazoongozwa na Umoja wa Afrika (AU), Fu Cong, mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa amesema jana Jumatatu.

    Kwenye hotuba yake katika mjadala wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za kulinda amani, Fu amesema, kuimarisha uwezo wa Afrika katika kudumisha amani na utulivu na kuongeza uungaji mkono katika mipangilio ya kikanda barani Afrika ni mwelekeo muhimu wa UN katika kubadilisha muundo wake wa kulinda amani.

    China inaunga mkono utoaji wa msaada wa kifedha ambao ni wa kutosha, unaotabirika na endelevu kwa operesheni za kulinda amani zinazoongozwa na AU”, amesema, akiongeza kuwa “tunatazamia mipangilio ya mfumokazi ulioanzishwa kwenye azimio la Baraza la Usalama Namba 2719 kuanza kutumika mapema”

    Huku akibainisha kuwa, Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefanyika Beijing wiki iliyopita, Fu amesema, China itashirikiana na Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kutekeleza hatua kumi za ushirikiano kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa, ambao unahusisha Mpango wa utekelezaji wa usalama wa pamoja.

    Amesema kwamba, China itachukua hatua kuiunga mkono Afrika katika kujenga uwezo wa jeshi na ulinzi, kutoa mafunzo kwa askari na maofisa wa jeshi na polisi na wale wa utekelezaji wa sheria kutoka Afrika na kutekeleza “Hatua za kufanya Afrika isiwe na mabomu ya kutega ardhini”.

    “China siku zote ni mwenzi mzuri wa Afrika kushirikiana bega kwa bega katika kutafuta maendeleo yenye sifa bora na usalama zaidi” Fu amesisitiza.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha