<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Singapore

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 10, 2024

    Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akifanya mazungumzo na mwenzake wa Singapore Vivian Balakrishnan mjini Beijing, China, Septemba 9, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

    Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akifanya mazungumzo na mwenzake wa Singapore Vivian Balakrishnan mjini Beijing, China, Septemba 9, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

    BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Singapore Vivian Balakrishnan mjini Beijing siku ya Jumatatu ambapo amesema kwamba, zikiwa ni nchi mbili zinazofanya kazi kwa ajili ya utulivu, China na Singapore zinahitaji kuimarisha uratibu na mawasiliano ya kimkakati katika Dunia yenye misukosuko.

    Huku akisema kuwa China na Singapore zote zina ajenda muhimu za kisiasa za nchini mwao mwaka huu na zinapiga hatua thabiti kuelekea malengo yao husika ya maendeleo, Wang ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema pande hizo mbili zimefanya kazi kwa ukaribu na kujifunza kutoka kwa kila mmoja, zikitoa msukumo muhimu kwa maendeleo ya ujenzi wao wa mambo ya kisasa.

    “China inapenda kuimarisha kazi ya kuunganisha mikakati ya maendeleo na Singapore, kutekeleza kihalisi ushirikiano wa pande zote wenye sifa bora na kuelekea siku za baadaye ulioanzishwa na viongozi wa pande hizo mbili, na kutoa mchango mpya kwenye amani, utulivu na maendeleo ya kikanda” Wang amesema.

    Amesema, pande hizo mbili zinapaswa kutumia vizuri mifumo ya mazungumzo katika ngazi zote na katika Nyanja mbalimbali, na kutumia vizuri sera yao ya kusameheana visa, na kuzidisha ujenzi wa jumuiya ya China na ASEAN yenye mustakabali wa pamoja, ili kuvutia nguvu kubwa zaidi za pamoja na kuingiza msukumo endelevu kwenye mafungamano ya kikanda na utandawazi wa uchumi.

    Kwa upande wake Balakrishnan amesema kwamba, Singapore inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja na inapinga kithabiti “Taiwan ijitenge na China”.

    Amesema Serikali mpya ya Singapore inapenda kutumia miaka 35 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Singapore na China mwaka ujao kama fursa ya kujiandaa kwa mawasiliano ya ngazi ya juu na kupanua ushirikiano jumuishi.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha