<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Ofisa wa Zimbabwe asema China ni chanzo kikuu cha uwekezaji wa kigeni nchini humo

    (CRI Online) Septemba 11, 2024

    Ofisa mwandamizi wa Zimbabwe Bw. William Manungo amesema, nchi hiyo inashuhudia ongezeko la uwekezaji, huku China ikichangia kwa kiasi kikubwa katika uwekezaji wa kigeni nchini humo.

    Bw. Manungo amesema hayo mjini Harare kando ya jukwaa la wadau wa idara ya uwekezaji na maendeleo ya Zimbabwe ZIDA, huku akiongeza kuwa China bado ni mwenzi mkuu wa uwekezaji wa Zimbabwe, hasa katika sekta za madini na uzalishaji viwandani.

    Pia amesema, uwekezaji wa China umejikita katika uchimbaji wa madini, lakini mbali na sekta hiyo, ushirikiano kati ya Zimbabwe na China pia umeshuhudia uwekezaji mkubwa katika uhusiano wa kiwenzi na serikali kwenye sekta ya uchukuzi, nishati na nyinginezo.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha