<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Idara ya Umoja wa Afrika yakaribisha uungaji mkono wa China kwa kilimo cha Afrika

    (CRI Online) Septemba 12, 2024

    Wakala maalum wa Umoja wa Afrika unaosimamia ujenzi wa uwezo umekaribisha ahadi ya China kuunga mkono Afrika kuendeleza kilimo na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

    Kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Beijing wiki iliyopita, China iliahidi kupanua ushirikiano na Afrika na kutekeleza hatua kumi za kiwenzi katika miaka mitatu ijayo.

    Katika sekta ya kilimo, China imeahidi kuunga mkono maendeleo ya kilimo kupitia mapendekezo mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa vituo vya kielelezo vya kilimo, kutuma wataalamu wa kilimo wa China na kuanzisha muungano wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia wa kilimo kati ya China na Afrika.

    Katibu mtendaji wa Mfuko wa ujenzi wa uwezo wa Afrika (ACBF) wenye makao makuu huko Harare, Bw. Mamadou Biteye, amesema Afrika imenufaika kutokana na ujuzi, uvumbuzi na utaalamu wa wataalamu wa kilimo wa China.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha