<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    China yaipa kipaumbele Saudi Arabia katika diplomasia ya jumla hususan Mashariki ya Kati

    (CRI Online) Septemba 13, 2024

    Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang Jumatano alisema China inaweka kipaumbele kuendeleza uhusiano na Saudi Arabia katika diplomasia yake ya jumla hususan diplomasia yake ya Mashariki ya Kati.

    Li alisema hayo alipokutana na Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia ambaye pia ni Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mohammed bin Salman Al Saud na kuendesha kwa pamoja Mkutano wa Nne wa Kamati ya Pamoja ya Ngazi ya Juu kati ya China na Saudi Arabia.

    Alisisitiza kuwa chini ya uongozi wa kimkakati wa viongozi wa nchi mbili, China na Saudi Arabia zinashikilia kuheshimiana na kuaminiana, kufanya ushirikiano wa kunufaishana, kufundishana na kuelewana, uhusiano kati ya pande mbili unaendelea kwa kasi na kwa kina katika pande zote, na ushirikiano kwenye sekta mbalimbali umepata matunda mengi.

    Kwa upande wa Saudi Arabia, Mohammed alisema uhusiano kati ya Saudi Arabia na China unadumisha maendeleo yenye kiwango cha juu, nchi hizo mbili ni wenzi wa kimkakati wa pande zote wa kutegemeka.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha