<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Reli ya China-Laos yashughulikia mizigo ya bidhaa yenye uzito wa tani milioni 10

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2024

    Picha hii iliyopigwa Agosti 9, 2022 ikionyesha malori ya usafirishaji wa bidhaa za kuvuka mpaka katika Stesheni nchini Laos ya Vientiane Kusini ya Reli ya China-Laos. (Picha na Kaikeo Saiyasane/Xinhua)

    Picha hii iliyopigwa Agosti 9, 2022 ikionyesha malori ya usafirishaji wa bidhaa za kuvuka mpaka katika Stesheni nchini Laos ya Vientiane Kusini ya Reli ya China-Laos. (Picha na Kaikeo Saiyasane/Xinhua)

    KUNMING - Reli ya China-Laos hadi sasa imeshughulikia mizigo ya bidhaa zenye uzito wa tani zaidi ya milioni 10 zinazoagizwa na kuuzwa nje tangu ilipoanza kufanya kazi rasmi Desemba 2021, ambapo bidhaa hizo zina thamani ya yuan takriban bilioni 40.77 (kama dola za Marekani bilioni 5.74) kwa jumla, hadi kufikia siku ya Jumatatu wiki hii, takwimu za forodha zilizotolewa jana Jumanne zinaonyesha.

    Bidhaa zinazosafirishwa kupitia reli hiyo zimepanuka kutoka aina 500 za awali hadi aina zaidi ya 3,000 hivi sasa, shukrani kwa mfululizo wa hatua zinazotekelezwa na Idara ya Forodha ya Mji wa Kunming, kama vile ujenzi wa bandari inayotumia teknolojia za kisasa.

    Katika miezi minane ya kwanza ya Mwaka 2024, reli hiyo ilishughulikia mizigo ya bidhaa zenye uzito wa tani milioni 3.58 zilizoagizwa na kusafirishwa nje ya nchi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 22.8 kuliko lile la mwaka uliopita.

    Ikiwa ni alama ya mradi wa ushirikiano wa sifa bora wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, Reli ya China-Laos yenye urefu wa kilomita 1,035 inaunganisha Kunming, mji mkuu wa Mkoa wa Yunnan kusini-magharibi mwa China, na mji mkuu wa Laos, Vientiane.?

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha