Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa salamu za pongezi kabla ya Siku ya mavuno ya wakulima wa China
BEIJING – Kabla ya kuwadia kwa Siku ya saba ya mavuno ya wakulima wa China iliyoadhimishwa Jumapili, Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), alitoa salamu za pongezi na kutakia mema akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC kwa wakulima na makomredi wanaofanya kazi za kilimo na zile za mstari wa mbele vijijini kote China.
Katika salamu hizo, Rais Xi amesema licha ya athari mbaya za majanga ya asili na changamoto nyingine mwaka huu, China imepata ongezeko la nafaka za majira ya joto na kuhakikisha uzalishaji tulivu wa mpunga wa mapema, na inatarajia kupata mavuno ya nafaka katika mwaka mzima, hali ambayo itatoa uungaji mkono mkubwa wa kuendeleza na kuimarisha ufufukaji na uboreshaji wa uchumi pamoja na kuhimiza maendeleo yenye sifa bora.
Amesisitiza kuwa ili kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, ni muhimu kuimarisha kila wakati msingi wa kilimo na kuhimiza ustawishaji wa pande zote wa vijijini.
“Kamati za Chama na serikali katika ngazi zote zinapaswa kutekeleza vizuri maamuzi na mipango ya Kamati Kuu ya CPC kuhusu kilimo, vijiji na wakulima, kujifunza na kutumia uzoefu wa Miradi ya kujenga na kuboresha kwa ufanisi mazingira ya kufaa kwa uzalishaji mazao na kuishi maisha vijijini, na kuhakikisha ipasavyo hali tulivu na salama ya utoaji wa nafaka na mazao muhimu ya kilimo” amesema.
Vile vile ni muhimu kuendelea kuimarisha na kupanua mafanikio ya kupunguza umaskini, na kufanya kila juhudi kuimarisha faida za kiuchumi za kilimo, kuongeza mapato ya wakulima, na kuongeza hamasa zaidi vijijini, ili kuleta manufaa halisi kwa wakulima, amesema.
Ameeleza, inatarajiwa kwamba wakulima na watu kutoka sekta nyingine nchini kote watachukua hatua za kubadilisha mpango wa ustawishaji vijijini kuwa hali halisi hatua kwa hatua, ili kuweka msingi wa kuleta mambo ya kisasa kwenye kilimo na maeneo ya vijijini na pia kwa ajili ya kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu katika kilimo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma