Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa wito wa kuharakisha maendeleo ya mambo ya anga ya juu ya China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 23, 2024. (Xinhua/Ju Peng)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumatatu katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing alipokutana na wajumbe wa wanasayansi na wahandisi walioshiriki katika utafiti na maendeleo ya kazi ya chombo cha uchunguzi wa mwezi cha Chang'e-6 amewatia moyo wataalamu na wafanyakazi katika nyanja za usafiri kwenye anga ya juu za China kuendelea na juhudi zaidi na kuharakisha maendeleo ya mambo ya usafiri wa anga ya juu.
Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amesisitiza kwamba mafanikio ya mradi wa utafiti wa mwezi yanabeba hekima na bidii za vizazi kadhaa vya wataalam wa China, na yameonesha mafanikio makubwa ambayo China imepata katika kujitegemea kisayansi na kiteknolojia katika miaka ya hivi karibuni.
Ametoa wito wa kuenzi moyo wa utafiti wa mwezi, ukiwa na umaalum wa "kufuata ndoto, kuthubutu kuchunguza, kushirikiana kuzishinda changamoto, na kufanya ushirikiano wenye manufaa na kupata maendeo kwa pande zote," ili watu wote wa China kuongeza zaidi kujiamini na kujivunia kwa taifa lao la China, na kukusanya nguvu kubwa kwa ajili ya kuhimiza kwa pande zote ujenzi wa mambo ya kisasa ya China na kufikia ustawishaji wa kitaifa.
Ameeleza kuwa chombo cha Chang'e-6, kwa mara ya kwanza katika historia ya binadamu, kilikusanya sampuli kutoka upande wa mbali wa mwezi, na kupata mafanikio mapya ya teknolojia kadhaa muhimu, ikionesha mafanikio mengine ya kihistoria kwenye juhudi za China katika anga ya juu na vilevile katika sayansi na teknolojia. Amesema, hii ni hatua muhimu kwa mradi wa utafiti wa mwezi wa China.
Rais Xi amesisitiza kuwa katika miaka 75 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, mambo ya anga ya juu yamekua kutoka kuwa dhaifu hadi kuwa imara, na kupata maendeleo ya kihistoria ya sifa bora ya hali ya juu iliyo ya kupiga hatua kubwa.
Amesema kuwa anga za juu ni eneo la pamoja la binadamu, na utafiti wa anga ya juu ni mambo ya pamoja ya binadamu. Amesema, mradi wa utafiti wa mwezi daima umekuwa ukifuata kanuni za usawa, kunufaishana, kutumia kwa amani na kufanya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote ili kupata maendeleo kwa pamoja.
Chombo cha utafiti wa mwezi cha Chang'e-6 kilirushwa kwenda anga ya juu kutoka China Mei 3. Mnamo tarehe 25, Septemba, chombo kirejeshaji cha Chang'e-6 kilitua kaskazini mwa China, na kurudisha sampuli zenye uzito wa gramu 1,935.3 kutoka upande wa mbali wa mwezi.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akikutana na wajumbe wa wanasayansi na wahandisi walioshiriki katika utafiti, uundaji na ufanikishaji wa chombo cha utafiti wa mwezi cha Chang'e-6, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 23, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akikutana na wajumbe wa wanasayansi na wahandisi wa anga ya juu walioshiriki katika utafiti, uundaji na ufanikishaji wa chombo cha utafiti wa mwezi cha Chang'e-6, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 23, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akitazama sampuli kutoka kwenye mwezi na maonyesho ya mafanikio ya miaka 20 ya mradi wa utafiti wa mwezi, Septemba 23. (Xinhua/Xie Huanchi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma