Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa wito wa kuendelea kuhimiza mshikamano wa makabila vizazi hadi vizazi
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping kwenye barua ya majibu kwa watu wa vizazi vya wajumbe wa makabila mbalimbali waliojenga mnara Mwaka 1951 katika Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China na kula kiapo cha uaminifu cha kuendelea kuwa wamoja na kufuata Chama, amesisitiza umuhimu wa kuendelea na juhudi za kuhimiza mshikamano wa makabila kizazi hadi kizazi.
Rais Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesema katika barua hiyo kuwa, katika zaidi ya miaka 70 iliyopita, watu wa makabila yote ya China wamefuata Chama na kushikamana kwa kufanya juhudi mbalimbali, na wamepata mafanikio ya kihistoria katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya maeneo ya mpakani.
Huku Rais Xi akiliita taifa la China kuwa ni "familia kubwa ya makabila 56 yanayopendana na kujaliana," amesisitiza kwamba watu wa makabila yote wanapaswa kuongeza uelewa kuhusu jumuiya ya watu wote wa taifa la China na kufanya juhudi kwa ajili ya umoja wa taifa na maendeleo ya makabila mbalimbali.
Mnamo Mwaka 1950, wajumbe wa makabila tofauti huko Pu'er, Yunnan, walialikwa Beijing kushiriki kwenye sherehe za kuadhimisha mwaka wa kwanza tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Januari 1, 1951, watu wa Pu'er walifanya mkutano wa kula kiapo kujenga mnara huo kwa mujibu wa desturi zao waawkilishi jumla ya 48 walitia saini majina yao kwenye mnara huo.
Wawakilishi wa vizazi vyao hivi karibuni walimwandikia barua Rais Xi, wakimjulisha kuhusu hali ya maisha ya watu wa jamii za makabila madogomadogo chini ya uongozi wa Chama.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma