<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Tamasha la Muziki lafanyika DRC ili kuhimiza Amani katika eneo la Maziwa Makuu

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2022
    Tamasha la Muziki lafanyika DRC ili kuhimiza Amani katika eneo la Maziwa Makuu
    (Picha zinatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

    Tamasha kubwa la muziki limefanyika huko Goma, mji mkubwa ulioko Kaskazini Mashariki mwa DRC, kufuatia Tamasha la Muziki la Amani kurejea wikendi iliyopita, pamoja na janga la UVIKO-19 linaloendelea na migogoro ya kivita isiyoisha kwa miongo mingi.

    Chini ya kaulimbiu yenye matumaini “Kucheza kwa Mabadiliko, Kuimba kwa Amani,” Tamasha hilo la muziki la amani limekuwa likiwaunganisha wasanii wa Afrika ili kuwaleta pamoja watu wa eneo la Maziwa Makuu kwa kupitia muziki.

    Kurudi kwa Tamasha la Muziki

    Pamoja na kuwepo kwa janga la UVIKO-19, tamasha hilo baada ya kusimamishwa kwa mwaka mzima limerudi tena Goma, mji wenye idadi kubwa ya wakazi na ulioko karibu na mipaka kati ya DRC na Rwanda, Burundi na Uganda.

    Tamasha la mwaka huu likiwa na mada ya “Jishirikishe, tushiriki pamoja” limerudi Ijumaa wiki iliyopita, baada ya kufutwa mnamo 2021 kwa sababu ya hatua za kudhibiti UVIKO-19. Furaha iko kila pembezoni kwenye mji huo, huku wahudhuriaji kutoka ndani na nje ya DRC wakihitaji majibu hasi ya kipimo kimoja cha UVIKO-19 kwa ajili ya kushiriki wikendi hiyo iliyojazwa na muziki na dansi.

    Tamasha hilo lilifanyika kwa mara ya kwanza mnamo 2013, na kila mwaka hufanyika kwa siku tatu mfululizo Mwezi wa Februari. Waandaaji wa tamasha hilo wamesema, vijana 10,000 hivi kutoka Goma na mji wa karibu wa Gisenyi nchini Rwanda wameshiriki kwenye tamasha hilo, ambalo linajumuisha wasanii wa rumba na rap jukwaani.

    “Nimefurahi sana,” alisema Mumbere Mbondi, shabiki mkubwa wa tamasha hilo kutoka Goma, akionesha furaha yake kuwa tamasha hilo la muziki limepata mafanikio yasiyo rahisi baada ya kurejea. “Mwaka huu waandaaji wamejitahidi kadri wawezavyo ili kuwezesha kufanyika kwa tamasha,” alisema Mbondi.

    Wimbo wa Amani

    Licha ya maonesho na burudani, tamasha hilo, ambalo lilifunguliwa Ijumaa iliyopita, lilikusudia kuleta watu kutoka hali mbalimbali pamoja kwa kupitia utamaduni katika eneo hilo la tamasha, hasa katika mji ambao umekuwa katika hali ya dharura kwa miezi 7 kutokana na kusumbuliwa na vita vya mara kwa mara.

    Hata kabla ya tamasha kufunguliwa, zaidi ya wasanii 20 kutoka eneo la Maziwa Makuu walikusanyika huko Goma kutunga wimbo maalumu wa Amani, ambao ulipangwa kuchezwa kwa mara ya kwanza kwenye tamasha.

    Kwa kuwa wimbo huo umeimbwa kwa lugha nyingi za eneo hilo, wasanii kutoka nchi tofauti waliamua kuacha mipaka ya nchi zao na kushirikiana kutunga wimbo huo ili kuwafanya watu wasahau tofauti zao za kiasili.

    “Huu ni wimbo wa undugu au amani. Maneno yake tumeyachagua kwa pamoja na wasanii kutoka jamii kadhaa za DRC, Rwanda na Burundi, yanaendana vizuri na umoja na masikilizano, na tumejitahidi sana,” alisema Thomas Lusango, msanii mwongozaji wa wimbo, akisisitiza kuwa wimbo huo utaimbwa kwa Lugha za Kiswahili, Kinyarwanda, Kirundi na lugha nyingine za asili katika eneo hilo.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha