<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Wasanii wa Uganda wachanganya muziki wa Kichina na Kiafrika ili kuimarisha uhusiano kati ya watu wa pande mbili

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 16, 2022
    Wasanii wa Uganda wachanganya muziki wa Kichina na Kiafrika ili kuimarisha uhusiano kati ya watu wa pande mbili
    Wasanii wa Uganda wakitumbuiza wakati wa kipindi cha kurekodiwa katika Kituo cha Taifa cha Utamaduni cha Uganda (UNCC) mjini Kampala, Uganda, Februari 10, 2022. Midundo mizito ya Kiafrika iliyounganishwa na toni za Kichina ndiyo aina mpya zaidi ya muziki ambayo wasanii wa Uganda wanaikuza ili kuimarisha uhusiano baina ya watu wa nchi hizo mbili. (Xinhua/Zhang Gaiping)

    KAMPALA - Nyimbo zenye mdundo mzito za Kiafrika zilizounganishwa na toni za Kichina ni aina mpya zaidi ya muziki ambayo wasanii wa Uganda wanakuza ili kuimarisha uhusiano kati ya watu wa nchi hizo mbili za China na Uganda.

    Katika mwezi mmoja uliopita, wasanii hao wamekuwa wakifanya mazoezi ya nyimbo maarufu za Kichina huku wakitaka kuwafikia watazamaji wa China.

    Wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ya Kiafrika, wakipiga ala za muziki za Kiafrika lakini wakiimba nyimbo za Kichina, wasanii hao wanaimba kuhusu uzalendo na upendo.

    John Bosco Katende, mkufunzi wa kundi hilo aliliambia Shirika la habari la China, Xinhua kwamba kufanya mazoezi ya kuimba kwa Lugha ya Kichina mwanzoni ilikuwa vigumu lakini kwa sababu mwendelezo wa mazoezi ya muda mrefu, wanamuziki hao waliweza kuzipatia noti kwa usahihi.

    "Ni uzoefu mpya kwa sababu ya lugha, lakini tunapoenda kwenye lugha ya muziki ni sawa tu kwamba unakuta Wachina wanatumia noti za juu katika nyimbo kwani Waganda, wengi wanatumia kipimo cha noti za chini," Katende anasema.

    Katende ambaye amekuwa mkufunzi kwa miaka 20 anasema anaamini kuwa kundi hilo sasa linaweza kufanya vyema kwenye jukwaa la China na pia kufanya maingiliano na wasanii wa China.

    “Tunatazamia kubadilishana sanaa, Waganda wanaokwenda China na Wachina wakija hapa wanatumbuiza,” anasema.

    Florence Nakijoba, mwalimu wa lugha ya Kichina anasema ilikuwa rahisi kwa wanamuziki hao kufahamu haraka kile alichowafundisha. Nakijoba, ambaye ni sehemu ya mpango wa Serikali ya Uganda wa kutoa mafunzo kwa walimu watakaofundisha Lugha ya Kichina katika shule za sekondari, amekuwa na jukumu la kuwafundisha wanamuziki hao nyimbo mbalimbali na maana zake.

    Josephine Mugerwa, mmoja wa watoa burudani na pia mwanamuziki maarufu ameliambia Xinhua kwamba China ni moja ya nchi zinazoendelea kwa kasi duniani na hivyo kuimarisha uhusiano na nchi hiyo si tu kiuchumi au kisiasa bali pia kijamii lazima kupewe kipaumbele.

    "Tunajaribu kuimarisha urafiki kati ya Uganda na China, China imekuwa na uhusiano na Uganda kwa muda mrefu mzuri linapokuja suala la biashara lakini safari hii tunataka kuifanya kwa njia ya kijamii kupitia muziki. Inajisikia vizuri ukiona mtu mwingine kutoka nchi nyingine akiimba muziki wako," anasema.

    “Tunakuza uzalendo, tunataka kuitangaza Uganda nchini China ndiyo maana unaona tunaimba nyimbo za Kichina, tukiwa tumevaa mavazi ya Uganda,” anaongeza.

    Sam Okello, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya UNCC anasema kuna masomo kadhaa ya kujifunza kutoka China hasa wakati huu ambao mambo ya kisasa yanachukuliwa kama tishio la tamaduni za asili.

    "Nguvu ya China ilitokana na watu, China iliishi kama jamii iliyofungwa kwa muda mrefu na wakati inafunguliwa kwa Dunia, kila kitu kilifanyika kwa mujibu wa maadili ya kitamaduni ya China," Okello anasema.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha