<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Kazi ya kuibua Meli iliyozama miaka 160 iliyopita yaanza Shanghai (6)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 03, 2022
    Kazi ya kuibua Meli iliyozama miaka 160 iliyopita yaanza Shanghai
    Picha kutoka kwenye faili isiyoandika tarehe ikionesha mabaki ya kale ya kitamaduni yaliyogunduliwa katika Meli ya kale Yangtze No. 2 iliyozama katika Mji wa Shanghai, Mashariki mwa China.

    Kazi ya kuibua meli iliyozama miaka 160 iliyopita imeanza kufanyika Jumatano wiki hii. Meli hiyo ya kale iliyotengenezwa kwa mbao ni kubwa zaidi na iliyohifadhiwa vizuri zaidi mpaka sasa, ambayo iligunduliwa chini ya bahari nchini China. Katika meli hiyo iliyozama, kuna mabaki mengi ya kale ya kitamaduni, ilikuwa meli ya wafanyabiashara wakati wa utawala wa Mfalme Tongzhi (1862-1875) wa Enzi ya Qing ya China.

    Ikiwa imepewa jina la Meli ya kale ya Yangtze No. 2 iliyozama, meli hiyo iligunduliwa sehemu yenye kina cha mita 5.5 chini ya bahari kwenye pwani ya Hengsha Kaskazini Mashariki mwa Kisiwa cha Hengsha la eneo la Chongming la Shanghai, China. (Picha zinatoka Idara ya Mabaki ya Kale ya Kitamaduni ya Shanghai /Zikichapishwa na Xinhua) 

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha