Lugha Nyingine
Wanyama pori wanaohifadhiwa wa Tibet, Kusini Magharibi mwa China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2022
Picha iliyopigwa Aprili 10, 2022 ikionesha kundi la bata bukini wenye milia kichwani katika Wilaya ya Rutog, Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kusini Magharibi mwa China. |
Kutokana na kazi ya eneo hili ya kulinda viumbe hai anuwai, Tibeti imekuwa mahali pa kuishi vizuri kwa wanyama pori katika miaka mingi iliyopita.
Ikilinganishwa na takwimu iliyotolewa na Shirika la kulinda Wanyama Pori la eneo hili miaka ya 1990, idadi ya punda pori wa Tibeti imeongezeka kutoka 50,000 hadi 90,000 hivi.
Na idadi ya korongo wenye shingo nyeusi imeongezeka kuzidi 10,000 kutoka idadi ya awali ya 1000 hadi 3000, huku idadi ya yak pori imeongezeka hadi 10,000 hivi.
Wakati huo huo, katika miongo kadhaa iliyopita, idadi ya swala wa Tibeti imeongezeka kwa kasi kutoka 50,000 hadi zaidi ya 300,000.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma