<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping atumai uhusiano wa China na Ujerumani ulio wa utulivu, wa kiujenzi na kuogoza uoneshe umuhimu wake

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 10, 2022
    Rais Xi Jinping atumai uhusiano wa China na Ujerumani ulio wa utulivu, wa kiujenzi na kuogoza uoneshe umuhimu wake
    Rais Xi Jinping wa China akikutana na kufanya mazungumzo kwa njia ya video na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz hapa Beijing, mji mkuu wa China, Mei 9, 2022. (Xinhua/Li Xueren)

    BEIJING - Rais Xi Jinping wa China jana Jumatatu amefanya mkutano kwa njia ya video na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ambapo amesema kwamba ni muhimu sana kwa nchi hizo mbili kuufanya uhusiano kati yao ulio wa utulivu, wa kiujenzi na kuongoza ufanye kazi yake muhimu.

    Xi alibainisha mabadiliko yenye utatanishi yanayoendelea kutokea katika hali ya kimataifa na kuongezeka kidhahiri kwa matatizo na changamoto kwa usalama na maendeleo ya Dunia, na akasisitiza haja kubwa ya kuleta utulivu na uhakika zaidi katika zama zenye msukosuko na mabadiliko.

    Xi alisema, China na Ujerumani ni nchi zenye ushawishi mkubwa. Chini ya hali ya sasa, ni muhimu sana kwa nchi hizo mbili kudumisha ukuaji mzuri na thabiti wa uhusiano wa pande hizo mbili na kuufanya uhusiano huo ulio wa utulivu, wa kiujenzi na kuongoza ufanye kazi yake muhimu. Hii siyo tu kwamba itatumikia maslahi ya watu wa China na Ujerumani lakini pia itachangia kwa kiasi kikubwa amani na utulivu duniani.

    Xi amesisitiza kuwa uhusiano kati ya China na Ujerumani umeshuhudia maendeleo ya hali ya juu katika miongo mitano iliyopita, ambapo pande hizo mbili zimeendelea kwa pamoja na kuchangia mafanikio ya kila mmoja wao kwa kuzidisha ushirikiano wa kivitendo. “Hii kimsingi inachangiwa na kuhimiza kuheshimiana na kufanya ushirikiano wa kunufaishana, uzoefu wa thamani na kanuni muhimu ambayo inapaswa kuzingatiwa wakati wote” Xi alisema.

    Xi alisisitiza kwamba hakuna mabadiliko katika dhamira ya China ya kuendeleza uhusiano na Ujerumani; hakuna mabadiliko katika matakwa ya dhati ya China kwa ushirikiano wa karibu na Ujerumani; na hakuna mabadiliko katika imani ya China kwamba China na Ujerumani zinaweza kufanikisha mambo mengi makubwa kubwa kwa pamoja. Amesema, ni muhimu pande hizo mbili zikishikilia njia kuu ya mazungumzo na ushirikiano, kutumia vyema njia za mazungumzo na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na kufanya mazungumzo katika nyanja kama vile mabadiliko ya tabianchi, sera za uchumi mkuu, utulivu wa mambo ya fedha, usalama wa nishati, usalama wa chakula na utulivu wa minyororo ya viwanda na ugavi, ili kuboresha zaidi uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

    Xi alisema, pande hizo mbili zinapaswa kutafuta maeneo mapya ya ushirikiano na kushikilia kwa uthabiti ushirikiano wa pande nyingi, usimamizi wa Dunia nzima wa kufuata utaratibu huku Umoja wa Mataifa ukibeba jukumu kuu. Pia ameikaribisha Ujerumani kuunga mkono juhudi za China katika Pendekezo la Amani ya Dunia nzima na Pendekezo la Maendeleo ya Dunia nzima.

    Xi pia alisisitiza uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya na kueleza kwamba chini ya msukosuko wa siasa za kijiografia zilizopo, China inaunga mkono uhuru wa kimkakati wa Umoja wa Ulaya. Ameeleza kwamba, uhusiano wa China na Ulaya haulengi, hautegemei, au kudhibitiwa na upande wa tatu. “Haya ni makubaliano ya kimkakati ambayo pande zote mbili lazima zifuate kwa muda mrefu” amesema.

    Kwa upande wake Scholz alisema uhusiano wa Ujerumani na China yameendelea vizuri katika miaka ya hivi karibuni, na kutoa wito kwa pande hizo mbili kuendeleza desturi nzuri na kuhimiza mwelekeo mzuri wa uhusiano wa nchi hizo mbili.

    Alisema kwamba, Ujerumani itashirikiana na China katika kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia, kudumisha mawasiliano ya karibu na mabadilishano katika ngazi zote.

    Viongozi hao wawili pia wamezungumza na kujadiliana kwa kina na kwa uwazi kuhusu hali ya Ukraine. Katika hili Xi alisisitiza kuwa, China siku zote inasimama upande wa amani na kufanya hitimisho lake kwa kujiamulia kwa kuzingatia uzuri na ubaya wa kila jambo. Xi amesema upande wa Ulaya unahitaji kuonyesha uwajibikaji wa kihistoria na hekima ya kisiasa, kuzingatia utulivu wa muda mrefu wa Ulaya, na kuhimiza suluhisho kwa njia ya kuwajibika. 

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha