Lugha Nyingine
Kufuatilia watoto wa Pembe ya Afrika inayokabiliwa na ukame katika Siku ya Kimataifa ya Watoto wa Afrika (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 16, 2022
Picha hii ikionesha mtoto kwenye Kijiji cha Kilifi cha Kenya kinachokumbwa na ukame tarehe 23, Machi. (Picha/Xinhua) |
Tarehe 16, Juni ni siku ya kimataifa ya watoto wa Afrika, ambayo inalenga kuwafahamisha watu kuhusu balaa ya njaa, vita, umaskini, ugonjwa inayowakumba watoto wa Afrika. Mashirika ya uokozi wa kibinadamu likiwemo shirika la Umoja wa Mataifa, na mashirika mbalimbali ya hali ya hewa siku hizi yalitoa taarifa ya pamoja yakionya, pembe ya Afrika hivi sasa inakumbwa na ukame mbaya zaidi katika miongo kadhaa iliyopita kutokana na uhaba wa mvua kwa miaka minne mfululizo. Kwa mujibu wa ripoti za Somalia, Kenya na Ethiopia, katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu, idadi ya watoto wenye hali mbaya ya utapiamlo wanaohitaji matibabu imeongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma