<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi wa China awasili Uzbekistan kwa ziara ya kiserikali, kuhudhuria mkutano wa kilele wa SCO (3)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2022
    Rais Xi wa China awasili Uzbekistan kwa ziara ya kiserikali, kuhudhuria mkutano wa kilele wa SCO
    Rais Xi Jinping wa China akiwasili Samarkand kufanya ziara ya kiserikali nchini Uzbekistan na kuhudhuria Mkutano wa 22 wa Baraza la Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai (SCO), Septemba 14, 2022. (Xinhua/Li Xueren)

    SAMARKAND - Rais wa China Xi Jinping amewasili Samarkand, Uzbekistan Jumatano jioni ambapo atafanya ziara ya kiserikali nchini Uzbekistan na kuhudhuria Mkutano wa 22 wa Baraza la Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).

    Kwenye uwanja wa ndege, Xi alilakiwa kwa furaha na Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev, Waziri Mkuu Abdulla Aripov, Waziri wa Mambo ya Nje Vladimir Norov, Gavana wa Mkoa wa Samarkand, Erkinjon Turdimov na maafisa wengine wa ngazi ya juu.

    Mirziyoyev alifanya hafla kubwa ya kumkaribisha Xi kwenye uwanja wa ndege. Takriban bendera mia moja za mataifa ya China na Uzbekistan zilikuwa zikipepea kwa upepo. Zulia lenye urefu wa mita mia lilikuwa limezungukwa na wanajeshi waliokuwa wakitoa salamu za heshima. Marais hao wawili waliingia na kusimama kwenye eneo mahsusi la kutazama lililopambwa vizuri kuakisi umaalumu wa usanifu wa Uzbekistan. Shangwe zilitoka kwenye Karnay, ala ndefu ya kitamaduni ya upepo ya Uzbekistan, ikiwa ni ishara ya kukaribisha. Vijana wa eneo hilo, wakiwa wamevalia mavazi ya makabila , walikuwa wakiimba na kucheza kwa mpigo uliochangamsha zaidi kumkaribisha mgeni wa heshima.

    Katika hotuba yake ya maandishi, Xi akiwa kwa niaba ya serikali ya China na watu wake alitoa salamu za dhati na kuitakia kila la kheri serikali ya Uzbekistan na watu wake. Xi amesisitiza kwamba kwa zaidi ya miaka elfu mbili, urafiki kati ya China na Uzbekistan na watu wake bado unajaa nguvu na uhai.

    “Ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Uzbekistan umeelekeza kwenye kasi ya maendeleo, siyo tu kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili, bali pia kuhimiza amani, utulivu, ustawi na maendeleo ya eneo hilo.” Xi amesema.

    Ameeleza kuwa atafanya mazungumzo na Mirziyoyev kwa ajili ya kubadilishana maoni ya kina kuhusu kuimarisha ushirikiano wa pande hizo mbili, na kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa yenye maslahi ya pamoja, na kuandaa kwa pamoja muongozo wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Uzbekistan. Ameeleza kuwa, atakuhudhuria Mkutano wa SCO Samarkand, na kufanya kazi na pande zote ili kuendeleza Moyo wa Shanghai, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, na kuhimiza maendeleo thabiti na imara ya SCO.

    Akiwa ameandamana na Mirziyoyev, Xi alipitia chumba cha wageni mashuhuri kwenye uwanja wa ndege ambapo skrini ya kidijitali ilionyesha picha kubwa ya Xi yenye maneno "Karibu kwa Ukarimu Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Xi Jinping Kutembelea Uzbekistan" kwa lugha ya Kichina na Kiuzbeki.

    Xi alimuaga Mirziyoyev kabla ya kuondoka kutoka uwanjani hapo. Marais hao wawili walisisitiza tena mazungumzo rasmi kati yao yatafanyika leo Alhamisi na kukubaliana kuwa watabadilishana kwa kina maoni juu ya kuimarisha urafiki kati ya China na Uzbekistan. 

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha