<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Xi amtunuku tuzo ya nishani ya urafiki Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (2)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 01, 2022
    Xi amtunuku tuzo ya nishani ya urafiki Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam
    Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Rais wa China, na Nguyen Phu Trong, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, wakiwa kwenye mazungumzo ya chai baada ya hafla ya kukabidhi tuzo ya nishani iliyofanyika kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Oktoba 31, 2022. Xi Jinping amemtunuku Nguyen Phu Trong Tuzo ya Nishani ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China siku ya Jumatatu. (Xinhua/Yao Dawei)

    BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Rais wa China, Jumatatu amemtunuku Nguyen Phu Trong, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) Tuzo ya Nishani ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China.

    Hafla hiyo imefanyika kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing. Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na waziri wa mambo ya nje wa China, alisoma amri ya tuzo hiyo ya nishani.

    Xi amemkabidhi Trong nishani hiyo, akimsifu Trong kuwa mwana Marxist, na komredi wa karibu na rafiki wa dhati wa CPC.

    “Kwa umakini wake mkubwa na uhimizaji wa kibinafsi, urafiki wa jadi kati ya pande hizo mbili na nchi umeimarishwa, kuaminiana kisiasa kumeimarishwa, ushirikiano wa kivitendo umeimarika, na mabadilishano na kufundishana kwa pande zote yamezidi kuwa karibu,” Xi amesema.

    Amesema kuwa, nishani hiyo inawakilisha hisia za kirafiki za CPC na watu wa China kwa Trong na watu wa Vietnam, inaashiria urafiki mkubwa kati ya China na Vietnam kama "makomredi na ndugu", na inadhihirisha matumaini makubwa ya pande hizo mbili na mataifa hayo mawili kwa ajili ya mustakabali bora wa pamoja.

    Huku akieleza kuwa China na Vietnam ni majirani na marafiki wema "waliounganishwa na milima na mito, walio karibu kama midomo na meno," Xi amesema, nchi hizo mbili ni makomredi wenye nia moja na washirika wenye mustakabali wa pamoja unaojitolea kwa ajili ya amani na maendeleo ya binadamu.

    Kuhusu safari ya kuhimiza ujamaa wa kisasa wa nchi hizo mbili, Xi amesema CPC iko tayari kushirikiana na CPV inayoongozwa na Trong ili kurithi urafiki wa jadi ulioanzishwa na kuhimizwa kwa uangalifu na Mao Zedong, Ho Chi Minh na viongozi wengine wa kizazi cha zamani wa pande hizo mbili na nchi mbili, na kuongoza kwa pamoja uhusiano kati ya China na Vietnam ili kupata maendeleo makubwa zaidi.

    Kwa upande wake, Trong amesema anamshukuru kwa dhati Xi kwa kumtunuku nishani hiyo, ambayo inaonyesha kikamilifu hisia za urafiki wa CPC, serikali ya China na watu wa China kwa CPV, serikali ya Vietnam na watu wa Vietnam, pamoja na viongozi wa Vietnam. Pia ni msukumo mkubwa kwa kujitolea kwa muda mrefu kwa Vietnam kwa urafiki wa Vietnam na China.

    Amesema ni furaha kubwa kwake kukubali heshima hiyo, na atafanya kazi na watu wa Vietnam katika wadhifa wake kuendelea kufuata njia ya ujamaa, kuhimiza na kuimarisha uhusiano wa kirafiki wa Vietnam na China kama "makomredi na ndugu, " na kutambua kwa pamoja mustakabali mzuri.

    Trong pia ameeleza matumaini kuwa urafiki wa Vietnam na China utadumu milele, na kwamba uhusiano wa Vietnam na China utakuwa mfano mzuri wa uhusiano wa kimataifa kutoka kizazi hadi kizazi.

    Baada ya hafla ya utoaji tuzo, Xi na Trong walifanya mazungumzo ya chai kuhusu urafiki wa jadi na matarajio ya maendeleo kati ya vyama hivyo viwili na nchi hizo mbili. 

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha