<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Uganda na China zasherehekea uhusiano kati yao unaokua kwa mbio za mashua za dragoni (2)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 01, 2022
    Uganda na China zasherehekea uhusiano kati yao unaokua kwa mbio za mashua za dragoni
    Wachezaji wakipiga makasia wakati wa mashindano ya boti za dragoni kwenye Hifadhi ya Misitu ya Buloba, Wilaya ya Wakiso, Uganda, Oktoba 30, 2022. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

    WAKISO, Uganda - Kwa sauti ya ngoma iliyopigwa mbele ya mashua yao yenye umbo la dragoni, Emily Namuyomba na timu yake, Twekombe Women, walipiga makasia kwa juhudi zote kuwashinda wakimbiaji wengine katika mashindano ya mbio za mashua za dragoni yaliyofanyika Wakiso, Uganda siku ya Jumapili.

    Namuyomba na wachezaji wenzake walifuata mdundo wa mpiga ngoma huku umati wa watu kwenye Hifadi ya Misitu ya Buloba, umbali wa Kilomita 19 Magharibi mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala ukishangilia.

    Mbio hizo ziliashiria kurejea kwa Mashindano ya Boti za Dragoni nchini Uganda baada ya kusimama kwa miaka miwili kwa sababu ya janga la UVIKO-19 linaloendelea.

    Tamasha la Mashua za Dragoni mwaka huu, ambalo ni tamasha la jadi la Wachina, ni sehemu ya matukio ya maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uganda na China.

    China ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Uganda Tarehe 18 Oktoba 1962, siku tisa tu baada ya Uganda kupata uhuru kutoka kwa wakoloni wa Uingereza.

    Timu saba za Uganda na timu moja ya China zilichuana majini ikiwa ni ishara ya kukua kwa uhusiano kati ya watu wa China na Uganda.

    Mbali na maji, kwenye mwambao wa bwawa la maji lenye urefu wa mita 200, jamii ndogo ya Wachina na Waganda walishangilia washindani.

    Kwa mujibu wa waandaaji, umati mdogo ulialikwa kwa sababu ya hatua zinazoendelea za kuzuia UVIKO-19.

    Elly Kamahungye, kaimu mkurugenzi wa masuala ya kikanda na kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda amesema kufanya tamasha la mashua za dragoni nchini Uganda kunaimarisha uhusiano kati ya watu wa nchi hizo mbili. "Naamini hii siyo tu inatumika kama mashindano na mkusanyiko lakini pia inakuza uhusiano kati ya watu na utamaduni wa nchi mbili za China na Uganda."

    Patrick Ogwel, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, amesema washindani wengi walikuwa na wastani wa sekunde 50 katika mbio za umbali wa mita 200, wastani ambao hautofautiani sana na wastani wa kimataifa wa sekunde 39, na kuongeza kuwa kutokana na mazoezi zaidi, wakimbiaji wa Uganda wanaweza kufanya vizuri zaidi.

    Namuyomba ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua muda mfupi baada ya mbio zake kuwa hawezi kusubiri siku ambayo atachaguliwa kuiwakilisha Uganda kwenye jukwaa la kimataifa. Amesema ingawa mbio hizo nchini Uganda zinaongozwa na wanaume, wanawake pia wanaweza kushindana. 

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha