<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (2)

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2022
    Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
    Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anayezuru China kabla ya mazungumzo yao kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Novemba 3, 2022. (Xinhua/Zhai Jianlan)

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Alhamisi amefanya mazungumzo na Rais wa Tanzania anayezuru China, Samia Suluhu Hassan hapa Beijing Mji Mkuu wa China. Marais hao wawili wametangaza kuinua uhusiano baina ya nchi hizo mbili hadi kufikia ngazi ya wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote.

    Akiweka bayana kuwa Rais Samia ndiye mkuu wa kwanza wa nchi ya Afrika ambaye China imepokea baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Xi amesema inaonesha uhusiano wa karibu wa nchi hizo mbili na nafasi muhimu ya uhusiano wa China na Afrika kwenye mambo yote ya jumla ya kidiplomasia ya China.

    Rais Xi amekumbuka alipotembelea Tanzania Mwaka 2013 alipendekeza kanuni ya kuaminiana, matokeo halisi, upendo na udhati katika kuongoza ushirikiano wa China na nchi za Afrika. Sasa imekuwa sera ya msingi inayoongoza mshikamano na ushirikiano wa China na nchi nyingine zinazoendelea.

    “Chini ya mazingira hayo mapya, ukuaji mzuri wa uhusiano kati ya China na Tanzania siyo tu kwamba unahimiza maslahi ya pamoja na ya muda mrefu ya nchi hizo mbili, bali pia una umuhimu mkubwa katika kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya” Xi amesema.

    Xi amemweleza Rais Samia hali kuhusu Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC. Amemfahamisha kuwa kuanzia sasa kazi kuu ya CPC itakuwa kuwaongoza watu wa China wa makabila yote katika juhudi za kufikia lengo la pili la miaka 100 tangu kuanzishwa CPC la kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote na kuendeleza ustawi wa Taifa la China katika sekta zote kupitia njia ya maendeleo ya kisasa ya China.

    "Usasa haimaanishi Umagharibi," Xi amesema, huku akiongeza China tayari imepata njia ya maendeleo inayoendana na hali ya nchi yake yenyewe. Amesema, maendeleo ya mambo ya kisasa ya China yanategemea hali halisi ya China yenyewe, na umaalumu wake kwa muktadha wa China.

    Rais Xi amesema Chama cha CPC na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vinabeba majukumu ya kihistoria ya kujiimarisha, na Chama cha CPC kitapanua mabadilishano na ushirikiano na Chama cha CCM na kusaidia mitaala na uendeshaji wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere.

    Xi amesisitiza kuwa China inautendea uhusiano wake na Tanzania kwa mtazamo wa kimkakati na daima itakuwa rafiki mwaminifu wa Tanzania. Kwa kutazama siku za mbeleni, Xi amesema pande hizo mbili zinapaswa kuendeleza urafiki na ushirikiano kote kote, kwa kuzingatia wenzi wa ushirikiano wa kimkakati na wa kina kati ya China na Tanzania.

    “China inaiunga mkono kwa dhati Tanzania katika kushikilia mamlaka yake, usalama na maslahi yake ya maendeleo, na katika kuchunguza njia ya maendeleo inayolingana na hali ya Tanzania. China na Tanzania zitaendelea kuunga mkono masuala yanayohusu maslahi ya msingi ya kila mmoja na mambo yanayohusu mambo makuu,” amesema Xi.

    Xi pia ameeleza mpango wa China wa kuongeza uagizaji wa bidhaa maalumu kutoka Tanzania, na kueleza kuwa maendeleo endelevu ya China yataleta fursa mpya kwa Afrika.

    Kwa upande wake Rais Samia huku akieleza kuwa amefurahishwa na kuheshimiwa kualikwa kutembelea China mara baada ya kumalizika kwa mafanikio kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, amesema ziara hiyo ni uthibitisho wa kiwango cha juu cha uhusiano kati ya Tanzania na China.

    Amesema, Tanzania inaiona China kama rafiki mkubwa wa kweli na itakuwa mshirika wa kutegemewa wa China siku zote. Ameongeza kuwa kwa kuingia kwenye ngazi ya wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote, Tanzania itashirikiana na China kuimarisha ushirikiano wa kivitendo katika sekta mbalimbali, kuupeleka uhusiano kwenye kiwango kipya, na kuugeuza kuwa mfano wa uhusiano wa Afrika na China katika zama mpya.

    Rais Suluhu pia amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuiunga mkono China kwa dhati katika masuala yanayohusu Taiwan, Xinjiang, Hong Kong na maslahi mengine ya msingi ya China. 

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha