<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping akutana na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 16, 2022
    Rais Xi Jinping akutana na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron
    Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Bali, Indonesia, Novemba 15, 2022. (Xinhua/Shen Hong)

    BALI, Indonesia - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumanne asubuhi.

    Rais Xi alisema katika miaka mitatu iliyopita viongozi hao wawili wamefanya mawasiliano ya karibu kwa njia mbalimbali, kudumisha mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ufaransa na kuwezesha ushirikiano muhimu wa nchi hizo mbili kupata maendeleo mazuri.

    Akielezea kwamba Dunia ya leo imeingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko, Xi amesema kuwa, zikiwa nguvu mbili kuu katika dunia hii yenye ncha nyingi, China na Ufaransa na China na Ulaya zinapaswa kushikilia moyo wa kujitawala na kujiamulia, kufungua mlango na kufanya ushirikiano, kuhimiza uhusiano baina ya nchi hizi mbili uendelee kwa utulivu na kupata maendeleo endelevu katika njia sahihi, na kuingiza utulivu na nguvu chanya duniani.

    Huku akisisitiza dhamira ya China ya kuhimiza kufungua mlango kwa kiwango cha juu na kuendeleza Maendeleo ya Kisasa ya China, Xi amesema juhudi hizi zitaipa Ufaransa na nchi nyingine fursa mpya.

    Rais Xi amesema, pande hizo mbili zinahitaji kufanya mipango ya ngazi ya juu kwa ajili ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili kwa mtazamo wa siku zijazo, kuheshimu maslahi ya msingi ya kila upande na mambo yanayohusu mambo makuu, kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji, na kuhimiza ushirikiano kwenye maeneo ya jadi upate maendeleo mapya siku hadi siku, huku zikitafuta kwa juhudi uwezo wa kufanya ushirikiano katika sekta za nishati ya kijani, uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia na maeneo mengine.

    “China inatumai kuwa Ufaransa itawapa wafanyabiashara wa China huko mazingira ya biashara yenye haki, usawa zaidi na yasiyo ya kibaguzi,” Xi ameongeza.

    Xi amesema China inatumai Ufaransa itahimiza Umoja wa Ulaya kuendelea kufuata sera ya kujiamulia yenye hamasa kwa China.

    Kwa upande wake, Macron ametoa pongezi za dhati kwa Rais Xi kwa kuchaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na kwa mafanikio kamili ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

    Ameeleza kuwa, Ufaransa na China zimejitolea kudumisha amani, maendeleo na ustawi wa uchumi duniani, na kupongeza njia ya China ya kufanya maendeleo ya kisasa.

    Huku akieleza kuwa Ufaransa inafuata sera huru ya mambo ya nje na inasimama dhidi ya makabiliano ya kambi, Rais Macron amesema katika hali ya kimataifa yenye utatanishi, Ufaransa inatarajia kuendelea kushirikiana na China katika kufuata moyo wa kuheshimiana, usawa na kunufaishana, kuongeza mawasiliano na mazungumzo ya ngazi ya juu, na kuimarisha ushirikiano katika maeneo kama vile biashara, uchumi, usafiri wa ndege na nishati ya nyuklia ya kiraia.

    “Ufaransa inakaribisha makampuni ya China nchini kwa ushirikiano wa kibiashara”, ameongeza.

    Pande hizo mbili pia zimebadilishana mawazo kuhusu hali ya Ukraine.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha