Lugha Nyingine
Tamasha la kufinyanga sanamu kwenye mchanga lafanyika kwenye ufukwe wa Bahari ya Mediterania wa Misri ili kuvutia vipaji vya Sanaa na watalii
ALEXANDRIA, Misri, - Tamasha la Kufinyanga Sanamu kwa Mchanga la Alexandria, ambalo ni la kwanza la aina yake lililoandaliwa na Jimbo la Alexandria la Misri ili kuhimiza utalii na vipaji vya vijana, lilihitimishwa Jumatano jioni.
Washiriki kumi na watatu kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria, Chuo Kikuu cha Matrouh na Chuo Kikuu cha Damietta walishiriki kwenye tamasha hilo.
Omniya Raafat, ambaye alikuwa mshindi wa tatu kwenye tamasha hilo kutoka Chuo Kikuu cha Matrouh, alishiriki uzoefu wake "bora" lakini "mgumu" wakati akifinyanga sanamu ya sokwe.
"Wakati nikifanyia kazi sanamu yangu ilianguka kutokana na upepo hali ambayo ilinikatisha tamaa sana. Lakini watu wengi walisema walipenda sanaa yangu kushiriki na kunitia moyo niendelee," alisema huku akisema zawadi aliyopata imefanya jitihada zake zote kuwa za manufaa.
Gavana wa Alexandria Mohamed Taher Elsherief amesema wanapanga kufanya tamasha hilo la sanamu kila mwaka.
"Ni mkusanyiko mzuri wa sanaa ambao unaangazia talanta za vijana wetu hapa Alexandria na majimbo mengine," gavana aliongeza.
Tamasha hilo liliwavutia watalii wengi waliokuja kuzistaajabu sanaa za mchanga zilizoonyeshwa huku wakifurahia mandhari ya bahari.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma