<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Beijing

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 15, 2023
    Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Beijing
    Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais Mahmoud Abbas wa Palestina kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Juni 14, 2023. Rais Xi amefanya mazungumzo na Rais Abbas mjini Beijing Jumatano. (Xinhua/Huang Jingwen)

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Beijing siku ya Jumatano.

    Viongozi hao wawili wametangaza kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Palestina.

    Rais Xi amesema China na Palestina ni marafiki wazuri na washirika wazuri wanaoaminiana na kusaidiana. Amesema China ni miongoni mwa nchi za kwanza kutambua Chama cha Ukombozi wa Palestina na Nchi ya Palestina.

    “China siku zote inaunga mkono kithabiti jihadi ya watu wa Palestina ya kurejesha haki zao halali za kitaifa na kufanyia kazi suluhu ya pande zote, yenye haki na ya kudumu juu ya suala la Palestina mapema,” Rais Xi amesema.

    Ameeleza kuwa, China inaunga mkono Palestina kuwa nchi mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa, itaendelea kuitetea Palestina na kutetea haki katika majukwaa mbalimbali ya ushirikiano wa pande nyingi, na itatoa msaada kadiri iwezavyo ili kusaidia kupunguza matatizo ya kibinadamu na ujenzi mpya wa Palestina.

    Ametoa wito kwa pande zote mbili za China na Palestina kuchukua uanzishwaji wa uhusiano wa wenzi wa kimkakati kama fursa ya kuendelea kusaidiana katika masuala ya msingi, kuendeleza ushirikiano katika maeneo mbalimbali, kuimarisha ushirikiano katika ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuharakisha mazungumzo kati ya China na Palestina juu ya makubaliano ya biashara huria, kubadilishana uzoefu juu ya uongozi wa kitaifa na kuendeleza urafiki wa jadi.

    Rais Xi ametoa pendekezo lenye vipengele vitatu kwa ajili ya kusuluhisha suala la Palestina. Kwanza suluhu ya msingi ipo katika kuanzishwa kwa nchi huru ya Palestina yenye mamlaka kamili ya nchi kwenye msingi wa mipaka iliyowekwa Mwaka 1967 na Jerusalem Mashariki ikiwa ni mji mkuu wake. Pili, mahitaji ya kiuchumi na kimaisha ya Palestina yanapaswa kutimizwa, na jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuongeza msaada wa maendeleo na msaada wa kibinadamu kwa Palestina na tatu, amesema ni muhimu kutilia maanani mwelekeo sahihi wa mazungumzo ya amani.

    Kwa niaba ya watu wa Palestina, Rais Abbas ameishukuru China kwa uungaji mkono wenye nguvu kubwa na msaada mkubwa usio na ubinafsi kwa muda mrefu kwa ajili ya jihadi ya watu wa Palestina ya kurejesha haki zao halali za kitaifa, na amesema China ni rafiki na mshirika mwaminifu.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha