Lugha Nyingine
Picha: Kuingia kwenye ukumbi wa kudumu wa Maonesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika
Maonesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yalifanyika kuanzia Juni 29 hadi Julai 2 huko Changsha mkoani Hunan, katikati mwa China. Licha ya eneo kuu la maonesha katika Kituo cha Kimataifa cha Maonyesho na Mikutano cha Changsha, maonesho hayo pia yamefanyika katika Eneo la Vielelezo vya kuhimiza Uvumbuzi wa Ushirikiano wa Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika. Inafahamika kwamba eneo kuu la maonesho ya kudumu lilifikia ukubwa wa mita za mraba 100,000, likiwa pamoja na sehemu mbili za meonesho ya mada kuu, mabanda matatu ya maonesho ya jumla, mabanda 34 ya maonesho ya nchi mbalimbali tofauti, ambapo nchi 53 za Afrika zote zimeonesha bidhaa zao kwenye maonesho hayo. Mabanda ya nchi za Afrika yalionesha hali mbalimbali ya nchi za Afrika, uhusiano wa pande mbili za Afrika na China, mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara, bidhaa maalum kama vile vinyago vya Afrika, maua mabichi, mazao ya baharini, Sanaa za usukaji wa majani ya ukindu, picha zilizochorwa kwa mafuta na bidhaa nyingine maalum.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma