Lugha Nyingine
Tamasha la Uvuvi kwenye?Mto Fuchun la Hangzhou lafanyika huko Hangzhou, China na uvuzi wa samaki?waanza tena baada ya kupigwa marufuku kwa miezi minne
Tamasha la Uvuvi kwenye Mto Fuchun la Hangzhou limefanyika kwenye Gati la Kale la Dongziguan katika Kitongoji cha Changkou kilichoko Wilaya ya Fuyang, Mji wa Hangzhou, mkoani Zhejiang, China Tarehe 3, Julai. Kwenye eneo la tamasha hilo, boti nyingi za uvuvi zilielea kuelekea katikati mwa Mto Fuchun, ili tu kuvua samaki wabichi zaidi wa mto huo.
Tarehe 1, Julai, marufuku ya uvuvi ya miezi minne kwenye sehemu ya Fuyang ya Mto Fuchun ilifikia mwisho rasmi, ikionyesha kuwa sasa Mto Fuchun unaweza kuvuliwa samaki kikamilifu.
Imeelezwa kwamba ili kulinda kikamilifu utagaji mayai, uanguaji mayai na ukuaji wa samaki wachanga na kuongeza ujazo wa asili wa rasilimali za samaki na kujijenga upya kwa mazingira ya ikolojia ya mto, Bonde la Mto Qiantang hutekeleza marufuku ya uvuvi kuanzia Machi 1 hadi Juni 30 kila mwaka. Marufuku hiyo hujumisha maeneo ya Mto Qiantang, Mto Fuchun, Mto Qujiang, Mto Lanjiang, Ziwa Qiandao, n.k. (Picha imetolewa na Idara ya Uenezi ya Kamati ya Wilaya ya Fuyang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma