Lugha Nyingine
Wakulima washughulikia kuvuna mazao ya mbegu za mayungiyungi huko Wilaya ya Quannan, Mkoa wa Jiangxi (4)
Wakati wa katikati ya majira ya joto, mazao ya mbegu za mayungiyungi yanayopevuka yanasubiri watu kuyachuma. Siku hizi, mazao ya mayungiyungi yamepevuka moja baada ya jingine katika kituo cha msingi cha upandaji wa mayungiyungi meupe cha Shilihetang ambacho kina eneo la hekta 20 la kupanda mayungiyungi meupe katika Mji mdogo wa Pitou wa Wilaya ya Quannan katika Mji wa Ganzhou, Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China. Wakulima wanashughulikia kuvuna mazao ya mbegu za mayungiyungi kuyatengeneza na kuyafunga kwa haraka, halafu wakayauza mtandaoni na nje ya mtandao ili kuongeza mapato.
Katika miaka ya hivi karibuni, kwa kutegemea mazingira bora ya kiikolojia na maliasili nyingi za kilimo, Mji mdogo wa Pitou umeendeleza shughuli za kilimo maalum za "kila kijiji kina mazao maalumu" kulingana na hali halisi ya vijijini ili kupata maendeleo chini ya uratibu wa upandaji wa kilimo na shughuli za utalii, na kukuza ustawishaji wa vijiji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma