<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Ziara ya Rais?Xi yaimarisha uhusiano kati ya China na Afrika Kusini katika "zama ya dhahabu", mguso wa BRICS kwa Ulimwengu wa Kusini

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2023
    Ziara ya Rais?Xi yaimarisha uhusiano kati ya China na Afrika Kusini katika
    Mabango ya Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Ushrikiano wa Nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) yakionekana katika mtaa huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 17, 2023. (Xinhua/Chen Cheng)

    JOHANNESBURG – Mwisho wa mwezi wa Agosti nchini Afrika Kusini unasifika kwa nyakati zake za mchana zenye kung'aa wakati jua la dhahabu la Afrika linapoosha mandhari katika kukumbatia kwake ukarimu.

    Inatumika kama msingi mzuri wa uhusiano unaostawi kati ya China na Afrika Kusini, ambao, kama alivyosema Rais wa China Xi Jinping, "umeingia katika 'zama ya dhahabu,' yenye matarajio mapana na mustakabali wenye matumaini."

    Mwaka huu inatimia miaka 25 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Afrika Kusini, na katika makala iliyochapishwa Jumatatu kwenye vyombo vya habari vya Afrika Kusini alipokuwa akianza safari yake kwenda kuhudhuria Mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za ushirikiano wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) mjini Johannesburg na kufanya ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini, Rais Xi amekumbuka "maendeleo ya hatua kwa hatua" ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kutoka ushirikiano hadi ushirikiano wa kimkakati, na kisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.

    "Ni moja ya uhusiano unaostawi zaidi wa nchi mbili katika ulimwengu wa nchi zinazoendelea," Rais Xi amesema katika makala yenye kichwa "Kuendesha Meli Kubwa ya Urafiki na Ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini kuelekea kwenye Mafanikio Makubwa."

    Si mara ya kwanza kwa Rais Xi kuuita urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini kuwa "meli kubwa." Mwaka 2015, kabla ya ziara yake ya kiserikali nchini humo, Rais Xi alisema katika makala iliyotiwa saini kwamba ushirikiano na urafiki wa pande mbili "umekua kutoka mashua ndogo hadi meli kubwa."

    Wakati Dunia inakabiliwa na hali nyingi za kutokuwa na uhakika na kuishi kupitia mabadiliko yenye kasi ambayo hayaonekana katika karne moja iliyopita, "sitiari hiyo bado inashikilia ukweli," amesema Sifiso Mahlangu, mhariri mkuu wa gazeti maarufu la Afrika Kusini, The Star, ambalo limechapisha makala zilizotiwa saini na Rais Xi wakati huu na ile ya Mwaka 2015.

    "Kwetu sisi Waafrika Kusini, ziara ya Rais Xi ni muhimu sana katika kustawisha na kuimarisha uhusiano wa pande mbili ... (ikiwa ni pamoja na) uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili," Katibu Mkuu wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) Fikile Mbalula amesema.

    Wasomi na wafuatiliaji wa BRICS wameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba kundi hilo limetetea dunia yenye ncha nyingi na ushirikiano wa pande nyingi tangu kuanzishwa kwake na limekuwa nguvu chanya, thabiti na ya kiujenzi katika masuala ya kimataifa, na kulifanya likaribishwe zaidi na Ulimwengu wa nchi za Kusini.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha