Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping awasili Johannesburg kuhudhuria Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa nchi za BRICS na kufanya ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini
Rais wa China Xi Jinping amewasili Johannesburg Jumatatu usiku kwa saa za Cape Town kuhudhuria mkutano wa 15 wa viongozi wakuu wa nchi za BRICS na kufanya ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini.
Ndege aliyopanda Rais Xi ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo huko Johannesburg, Afrika Kusini majira ya Saa 5 usiku. Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Naledi Pandor, na Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mambo ya Wanawake, Vijana na Walemavu, Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma walimkaribisha kwa furaha Rais Xi wakati akishuka ngazi ya ndege.
Rais Ramaphosa amekaribisha kwa furaha rais Xi kufanya ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini. Rais Xi amesema, anafurahi sana kuwasili tena Afrika Kusini, na anatarajia kubadilishana maoni na Rais Ramaphosa juu ya kuimarisha uhusiano kati ya China na Afrika Kusini na masuala mengine yanayofuatiliwa na pande zote.
Katika hotuba yake ya maandishi ilitolewa kwenye uwanja wa ndege, Rais Xi akiwa kwa niaba ya serikali na watu wa China ametoa salamu za dhati na kuitakia kila la kheri serikali ya Afrika kusini na watu wa nchi hiyo.
Rais Xi amesisitiza kuwa, mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 25 tangu uanzishwe uhusiano wa kidiplomasia wa China na Afrika Kusini, na uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote wa nchi hizo umeingia hatua mpya.
Amesema, kuimarisha na kuendeleza uhusiano huo siyo tu kunanufaisha watu wa nchi hizo mbili, bali pia kunatia utulivu zaidi kwa dunia yenye misukosuko. Amesema, anaamini kuwa, chini ya juhudi za pamoja za pande hizo mbili, ziara yake hiyo itakuwa na mafanikio mabubwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma